Makala
SHANGAZI AKUJIBU: Mke haniamini tena
Wanandoa wanaofarakana. Picha| Maktaba.
SWALI: Nina mke na nampenda sana. Lakini kuna jambo ambalo linatishia ndoa yetu. Haniamini kimapenzi. Kila nikipigiwa simu na mwanamke ni lazima tugombane. Ukweli ni kuwa sina mwingine. Nifanye nini?
Jibu: Hali yako ke wao inatokana na wivu na pia ni ishara kuwa anakupenda. Ili kumuondolea hofu, mruhusu kusikiliza mazungumzo kati yako na hao wanaokupigia simu. Hatimaye atajua ukweli na kutulia.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO