Habari za Kitaifa

HABARI ZA HIVI PUNDE: Watu 11 wafariki katika ajali ya ndege Kwale

Na WACHIRA MWANGI, CHARLES WASONGA October 28th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MAMLAKA ya Kusimamia Safari za Angani Nchini (KCAA) imethibitisha kuwa ndege moja iliyobeba abiria 12 ilianguka Jumanne, Oktoba 28, 2025 katika Kaunti ya Kwale..

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, KCAA ilisema kuwa ajali ilitokea mwendo wa saa mbili na nusu asubuhi ndege hiyo ilipokuwa ikisafiri kutoka Diani hadi Kichwa Tembo.

“Mamlaka ya Kusimamia Safari za Anga Nchini (KCAA) ingependa kuthibitisha kuwa ndege moja yenye nambari ya usajili 5Y-CCA, ikiwa safarini kutoka Diani hadi Kichwa Tembo, ilianguka katika 0530Z,” ikasema.

Kulingana  na KACC, ndege hiyo ilikuwa imebabe abiria 12 ajali hiyo ilipotokea.

“Ndege hiyo ilikuwa imebabe watu 12. Maafisa kutoka asasi husika za serikali tayari wamefika eneo la tukio kubaini chanzo cha ajali na athari zake,” mamlaka hiyo ikaongeza.

Maelezo kuhusu waathiriwa na manusura hayakuwa yametolewa kufikia wakati wa kuchapishwa kwa habari hii.