Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Kumbe ni binti ya mpenzi wangu wa zamani!
SWALI: Shikamoo shangazi. Nimeshangaa kugundua mpenzi wangu ni binti ya mwanamke aliyekuwa mpenzi wangu miaka kadhaa iliyopita. Nataka kumuoa na sijui mama yake akijua itakuwaje. Nahitaji ushauri wako.
Jibu: Hapo kuna shida. Nina hakika kuwa mama ya mpenzi wako akijua atafanya kila awezalo kuwatenganisha na ikibidi amwambie ukweli binti yake. Ni heri umwambie ukweli ili mvunje uhusiano wenu.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO