Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Binamu alinilazimisha tushiriki mapenzi naye
Picha ya wapenzi wawili baada ya ugomvi. Picha| Maktaba
SWALI: Nina miaka 18. Juzi nililimtembelea shangazi yangu mjini na kijana wake akanilazimisha tufanye mapenzi. Ninataka kumwambia mama yake lakini anatishia kujiua. Nifanye nini?
Jibu: Iwapo binamu yako pia ni rika yako, itakuwa vigumu kutatua jambo hilo kwa kuwa nyinyi bado ni watoto. Bila shaka anahofia ukifichua ataadhibiwa. Msamehe tu kisha umuepuke kabisa kwani umejua si mtu mzuri.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO