Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Mke wangu ametishia kuniua, nifanyeje?
Wanandoa waliotengana. Picha|Maktaba.
SWALI: Nina mke na watoto wawili. Mke wangu anapenda sana ugomvi na tunapigana karibu kila siku. Juzi tuligombana na kwa mara ya kwanza akanitishia maisha kwamba siku moja ataniua. Nipe ushauri.
Jibu: Tunaambiwa ndoa hudumishwa kwa kuvumiliana. Lakini kuna mambo mengine ambayo hayawezi kuvumiliwa. Kama mke wako amekuonya wazi kuwa siku moja atakuua, maisha yako yamo hatarini. Ningekuwa wewe ningejiondoa mara moja.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO