Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Halali kitandani tukikosana
Wanandoa wanaoonekana kukosana. PICHA|HISANI
SWALI: Hujambo shangazi. Mume wangu anapenda kulala sebuleni kila tukigombana. Sasa amejizoesha mpaka anasema “nimezoea sofa.” Je, ndoa yetu itadumu?
Jibu: “Nimezoea sofa” si kauli ya ndoa thabiti. Zungumzeni chanzo cha migogoro kabla sofa iwe kitanda cha kudumu.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO