Shangazi Akujibu

SHANGAZI AKUJIBU: Mke hapendi nikiwa kwa hii michezo ya video

Na SHANGAZI November 15th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Shikamoo shangazi. Mke wangu ananiita “mtoto mkubwa” kwa sababu napenda michezo ya video. Kila mara nikicheza ananikemea. Naomba ushauri.

Jibu: Michezo ya video si dhambi, ila usipitilize. Onyesha uwiano kati ya starehe na majukumu, naye ataelewa.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO