Shangazi Akujibu

Nimefutwa kazi, mipango yangu ya harusi taabani

Na SHANGAZI November 19th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Nilikuwa nimeanza kupanga sherehe kubwa ya harusi na mpenzi wangu. Lakini mpango huo umekatizwa baada ya kuachishwa kazi mwezi uliopita. Sijui nitamwambia nini mpenzi wangu. Nishauri tafadhali.

Jibu: Maana ya ndoa hasa ni wawili kuanza maisha pamoja kama mtu na mke wake. Harusi ni sherehe tu ya kuadhimisha ushirika huo. Mnaweza kufanya harusi miaka mingi baada ya ndoa. Mwambie ukweli kuhusu hali yako.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO