Shangazi Akujibu

Tumeishi pamoja miaka 2, sasa adai hana hisia kwangu

Na SHANGAZI November 16th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Nimekuwa na mpenzi kwa miaka miwili. Hata hivyo, kuna dalili kuwa penzi lake kwangu ni shingo upande. Juzi nilimuuliza na akaungama kuwa hana hisia kwangu lakini alishindwa kuniambia.

Jibu: Uhusiano usiokuwa na mapenzi kutoka pande zote mbili hauwezi kuendelea. Umejua ukweli kuwa mapenzi yenu ni ya hadaa. Kwa hivyo itabidi ujiondoe katika uhusiano huo ili utafute mapenzi ya dhati.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO