Shangazi Akujibu
Amekatiza mawasiliano!
Mteja akitumia simu ya mkono. PICHA|PEXELS
SWALI: Mpenzi wangu wa miaka miwili amekatiza mawasiliano kwa wiki mbili bila sababu. Nilimtumia ujumbe kumuuliza akaniambia nimpe muda afikirie. Inawezekana ameamua kuniacha?
Jibu: Ni wazi kuwa mpenzi wako ameamua kuvunja uhusiano wenu lakini hutaki kuona hilo kwa sababu umepumbazwa na penzi lake. Ni jambo gani anataka kufikiria ilhali mmekuwa wapenzi kwa miaka miwili?
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO