Aladwa ataka Winnie awe naibu kiongozi wa ODM
MBUNGE wa Makadara George Aladwa, sasa anataka Winnie Odinga ashirikishwe katika masuala ya kila siku ya ODM badala ya kutengwa huku uhasama wa ndani kwa ndani ukiendelea kukumba chama hicho cha upinzani.
Bw Aladwa, amependekeza Bi Winnie, mwanawe Raila atengewe wadhifa maalumu ndani ya ODM kumrithisha na kuendeleza siasa za babake.
Bi Winnie anahudumu kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) na ameonekana kutofautiana na Kiongozi wa ODM Dkt Oburu Oginga ambaye pia ni ami yake.
Wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya ODM, Bi Winnie alipendekeza Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC) liandaliwe, kutathmini na kutoa mwelekeo kuhusu ushirikiano wa ODM na Serikali Jumuishi hasa wakati huu ambapo Bw Odinga sasa hayupo.
“Tunahitaji kurudi kwa wananchi tuandae NDC na tuone ni nani watu wanataka kumchagua kusimamia uhusiano huo,” akasema Bi Winnie.
Kwa mujibu wa Bw Aladwa, mwana huyo wa ‘Baba’ anastahili kuwa mmoja wa manaibu kiongozi ODM.
“Haya ni maoni yangu kwamba ODM inastahili kubuni nafasi ya naibu kiongozi wa chama kwa Winnie kwa kuwa ni bintiye Raila na kama kijana, ataleta mbinu mpya ya kuvumisha chama,” akasema