Shangazi Akujibu

SHANGAZI AKUJIBU: Mke wa bosi amenipenda, nahofia kufutwa!

Na SHANGAZI November 26th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Kwako Shangazi. Jana tulikuwa na kikao cha wafanyakazi kuboresha mahusiano ya kikazi (team-building) na tukaanza kuzungumza na mke wa bosi wangu. Baadaye akanitafuta kwenye WhatsApp akisema alifurahia mazungumzo yetu. Ninahofia Bosi akijua atanifuta kazi! Naomba ushauri wako.

Jibu: Usijichimbie kaburi. Mjibu kwa heshima na uweke mipaka. Ukicheza na moto, ofisi itakuwa jivu.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO