Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Kila kitu kwa mpenzi ni ‘ex’ wangu hivi, ‘ex’ vile!
Mwanaume anayechiti mpenzi wake. Picha|Maktaba.
SWALI: Shikamoo Shangazi. Kila tukizungumza na mpenzi wangu, lazima ataje ex wake. Nimechoka kusikia habari kuhusu huyo mtu. Naona kama bado wanapendana.
Jibu: Mtu akimtaja ex mara kwa mara anaonyesha hajamsahau. Usigombanie nafasi ya pili. Chukua viatu vyako ukimbie.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO