Opta: Arsenal bado pazuri kushinda EPL licha ya sare; Man U wangali hawatoshi mboga
LICHA ya kudondosha alama mbili muhimu katika sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea hapo Novemba 30, 2025, Arsenal bado wanapigiwa upatu na kompyuta maalum ya Opta kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu 2025-2026.
Opta imewapa wanabunduki uwezo wa asilimia 78.69 wa kutawala ligi hiyo ya timu 20.
Hata hivyo, sare hiyo uwanjani Stamford Bridge inahisi kama nafasi muhimu iliyopotea kwa vijana wa kocha Mikel Arteta.
Chelsea walisalia wachezaji 10 baada ya Moisés Caicedo kumchezea vibaya Mikel Merino dakika ya 38, lakini bado vijana wa kocha Enzo Maresca ndio walifungua ukurasa wa mabao kupitia Trevoh Chalobah mapema kipindi cha pili.
Wanabunduki wa Arsenal walilazimika kutoka nyuma na mwishowe wakashindwa kutumia faida ya kuwa na mchezaji mmoja zaidi. Hiyo ni mara ya kwanza Arsenal kutoshinda mchezo wa Ligi Kuu baada ya mpinzani kupata kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza tangu Agosti 2010.
Badala ya kuimarisha pengo la pointi saba kabla ya kualika Brentford ugani Emirates hapo Desemba 3, Arsenal sasa wako mbele ya Manchester City kwa pointi tano baada ya mechi 13 za kwanza.
Hata hivyo, makadirio ya Opta yanaonyesha Arsenal watamaliza kileleni kwa pengo la pointi 11.
Kiwango chao cha pointi 81 kitafanana na kile Leicester walioibuka mabingwa msimu 2015–2016. Ni takwimu ya tano ya chini zaidi kwa bingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, lakini Arteta na kikosi chake hawatajali hilo iwapo watamaliza ukame wa miaka 21 bila taji.
Kwa upande mwingine, City wamepewa tu asilimia 11.43 ya kutwaa taji. Vijana wa Pep Guardiola wakimaliza na pointi 70 kama inavyotarajiwa, itakuwa idadi yao ya chini zaidi kama nambari mbili tangu Arsenal walipomaliza na pointi hizo msimu wa 2000–2001.
Chelsea wamepewa uwezekano wa asilimia 4.16 wa kushinda ligi, mbele ya Aston Villa (asilimia 1.93), Liverpool (1.92), Brighton (0.74), Newcastle (0.39), Crystal Palace (0.29), Manchester United (0.22), Brentford (0.09), Bournemouth (0.07), Tottenham (0.05), Fulham (0.01) na Sunderland (0.01%).
Licha ya nafasi ndogo ya kunyakua taji, Chelsea wanatabiriwa kumaliza nambari tatu, nao Liverpool katika nafasi ya nne. Blues huenda wakajikuta wakiridhika na kufuzu tu kushiriki Klabu Bingwa Ulaya badala ya kubeba ubingwa wa ligi mwezi Mei 2026.
Mbio za kuingia Klabu Bingwa Ulaya ni kali, na timu tano za juu zinatarajiwa kujikatia tiketi kushiriki michuano hiyo ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA).
Ushindi mwembamba wa Liverpool wa 1–0 dhidi ya West Ham umeimarisha ubashiri wa kumaliza nafasi ya nne. Pointi 63 zinazotarajiwa ni changamoto kwa kocha Arne Slot, lakini kufuzu kushiriki Klabu Bingwa Ulaya kutakuwa faraja ndogo.
Villa nao wanatarajiwa kukamilisha msimu na takriban pointi 63. Brighton na Palace pia wako karibu, na kufanya vita vya kumaliza kutoka nafasi ya nne hadi ya saba kuwa vigumu. Matokeo machache ya kushangaza yanaweza kubadilisha ramani ya Ligi ya Uropa.
Newcastle wanatabiriwa kumaliza nambari nane, kupanda kutoka nafasi ya 13 ya sasa. Opta wanaamini kikosi cha kocha Eddie Howe kitapata makali tena na kumaliza na pointi 58, sawa na Palace.
Vijana wa kocha Ruben Amorim wamepanda hadi nafasi ya tisa baada ya kutoka nyuma na kubomoa Palace. Brentford wanakamilisha 10-bora.
Kwa mashetani wekundu wa United, kurejea Klabu Bingwa Ulaya kutasubiri msimu mwingine, lakini ubashiri wa Opta unaonyesha wanaanza kujikwamua kutoka kwenye msimu wao mbovu wa kumaliza nafasi ya 15