Habari

Machifu wanasa chang’aa Mukuru

Na SAMMY KIMATU December 2nd, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MACHIFU wa eneo la Hazina wikendi walinasa chang’aa ambayo ilikuwa ikisafirishwa hadi mtaa wa mabanda wa Mukuru.

Naibu Kamishna wa Kaunti, Ibrahim Adan, alisema wakazi waliwaarifu machifu kuhusu usafirishaji huo na washukiwa wawili walitimka mbio na kunusurika kunaswa.

Bw Adan alishirikiana na Chifu Paul Mulinge na Naibu Chifu Vincent Ambunga na kunasa chang’aa hiyo iliyokuwa iuzwe kwa wanajamii mtaani.

Bw Adan alisema kuwa wakishirikiana na vyombo vya usalama, wataendelea kuimarisha vita dhidi ya matumizi ya mihadarati hasa kipindi hiki msimu wa likizo unapoingia.

Oparesheni dhidi ya dawa za kulevya itakuwa ikiendeshwa mitaa ya mabanda, vituo vya matatu, maeneo ya burudani na madanguro ya changáa.