Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Jirani atishia kunisingizia kwa mke eti namtaka
Mwanaume aliye na tamaa. Picha|Maktaba
SWALI: Kwako shangazi. Nimeoa na nina watoto wawili. Mwanamke jirani yetu amekuwa akinishawishi tuwe na mapenzi ya siri lakini nimekataa. Sasa anatishia kumwambia mke wangu eti mimi ndiye ninayemtaka. Nifanye nini?
Jibu: Inaonekana mwanamke huyo ameamua kutumia kifua kuvuruga ndoa yako. Lakini usikubali. Mwelezee mke wako kila kitu kisha mshirikiane kumkabili. Ukifanya hivyo utakuwa umetibua mpango wake.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO