Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Anapewa lifti kila siku, sijui ataniponyoka?
Mwanamke akiwa kwenye gari. Picha|Hisani
SWALI: Pokea salamu zangu shangazi. Mpenzi wangu anaishi mtaa jirani. Nimegundua kuna mwanamume amekuwa akimpa lifti kwa gari lake kwenda mjini karibu kila siku. Nahofia atatumia nafasi hiyo kunipokonya mpenzi. Nifanye nini?
Jibu: Hofu yako hiyo inaonyesha humwamini mpenzi wako. Hata kama mwanamume huyo ana nia kwake, itakuwa juu ya mpenzi wako kuamua kumkubali ama kumkataa. Ondolea mbali mawazo hayo.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO