Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Mpenzi wangu hataki nitembelee ndugu zangu
Familia ikifurahia wakati wao pamoja. Picha|Maktaba
SWALI: Vipi shangazi. Mpenzi wangu akiona ninaenda kuwaona ndugu zangu hupandwa na hasira. Anadai ninawapenda kumliko. Nifanyeje?
Jibu: Hiyo ni dalili ya woga wa kukupoteza. Weka mipaka kwa upendo lakini kwa uthabiti, ukimueleza kuwa unapenda familia yako na hiyo haimaanishi humpendi.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO