Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Mwanangu ameanza kuiba vifaa vidogo vidogo kwa nyumba na akana peupe
SWALI: Nimegundua mwanangu anaiba vifaa vidogo pale nyumbani. Kwa mfano, alichukua simu ya nyumbani akauza. Nilipomuuliza alikana kabisa kutoweka kwa kifaa hicho. Chakula kikibaki pia anaiba. Nifanyeje?
Jibu: Ni mapema sana kumuita mwizi. Chunguza chanzo cha tabia hiyo kwanza kisha rekebisha tabia yake mapema kwa mazungumzo na nidhamu ya upendo.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO