Mke ashtuka mumewe kutaka washiriki ufuska
MWANADADA mmoja mjini Malindi hapa aliye katika ndoa juzi alisema anapitia wakati mgumu baada ya mume wake kuanza kumshinikiza kushiriki mienendo ya kimapenzi asiyopenda.
Anadai mume wake amesisitiza kuhusu kubadilishana wapenzi na hata kupendekeza wanunue nyumba kubwa itakayoweza kutumika kwa karamu za ufuska.
Wakati huo huo, mwanadada mmoja mtaani Karen, Nairobi amefichua jinsi aliyekuwa mpenzi wake alivyodhani angeepuka adhabu baada ya kumtesa na kumkaba shingo mara kwa mara.
Hata hivyo, jombi hakujua kwamba, mwanamke huyo alikuwa ameweka kamera ndogo ya kunasa matukio ndani ya nyumba.
Kamera hiyo ilinasa matukio yote ya dhuluma, ikiwemo vitisho na ukatili aliokuwa akifanyiwa demu. Ushahidi huo ulimpa ujasiri wa kuchukua hatua na kujinusuru.
Alisema hakulenga kulipiza kisasi bali kujilinda na kuthibitisha ukweli.
Masimulizi yake katika mitandao ya kijamii yamezua mjadala kuhusu haja ya watu kuchanuka na kusaka mbinu za kujilinda dhidi ya unyanyasaji nyumbani.