Murkomen, Ogamba waliulizwa maswali mengi na wabunge
WIZARA za Usalama wa Ndani, Elimu, Barabara na Uchukuzi na Afya ni miongoni mwa zile zilizoulizwa maswali mengi zaidi na wabunge wakati wa kikao cha nne 2025.
Kikao hicho kilichoanza Februari hadi Desemba 4, 2025 kilishuhudia wabunge hao wakiulizwa maswali mbalimbali 130 kwa wizara 18.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na bunge kuhusu shughuli zote zilizofanywa katika mwaka huo, wizara ya usalama wa ndani iliulizwa maswali 26, wizara ya elimu 24, barabara na uchukuzi 23 huku wizara ya afya ikiwa na maswali 20.
Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Mambo ya Nje ilikuwa na maswali matano ambayo yote yalijibiwa, Hazina ya Taifa na Mipango ya Uchumi manne, kilimo na maendeleo ya mifugo, wizara ya maji, usafi wa mazingira yote pia yalikuwa na maswali manne.
Wizara ya Ardhi, Kazi za Umma, Nyumba na Maendeleo ya Miji, Masuala ya Vijana, Uchumi Ubunifu na Michezo zote ziliulizwa maswali mawili kila moja likitoka kwa wabunge.