UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Uhusiano wa Isimujamii na Jiografia
Na MARY WANGARI
JIOGRAFIA ni eneo lililotenganishwa kwa mipaka ya jamii ya eneo fulani linakuwa na namna tofauti ya utumiaji wa lugha kulingana na miaka yao.
Mwanaisimu jamii hana budi kuelewa jiografia ya eneo fulani ili kutambua miaka ya wazungumzaji wa lugha ingawa ni vigumu kutambua mipaka ya jamii kama si mhusika wa lugha hiyo au jamii hiyo hiyo. Hivyo basi hulazimika kutumia lugha kulingana na eneo fulani mfano eneo la wataita hutumia kitaita kutokana na eneo husika.
Kwa ujumla isimu jamii inasheheni mawanda mapana na mawanda finyu ambayo huchunguza uhusiano na tofauti za wazungumzaji wa lugha. Isimu jamii pia hutofautiana na taaluma nyingine katika maana na vipengele vingine lakini lugha na jamii ni dhana mbili ambazo haziwezi kamwe kutenganishwa. Hivyo basi isimu jamii na taaluma nyinginenzo humsaidia mwanaisimu anapokuwa akichunguza matumizi ya lugha katika jamii.
Mchakato wetu wa kudurusu na kuchunguza kwa kina dhana ya isimu hauwezi kukamilika pasipo kujifahamisha kuhusu istihahi mahsusi zinazotumika katika taaluma ya isimu. Istilahi hizo ni kama zifuatazo:
- Isimu Sinkronia
- Isimu Daikronia
Isimu Sinkronia na Isimu Daikronia
Katika Isimu Sinkronia, lugha huchunguzwa kwa kuangalia namna ilivyotumika katika kipindi fulani maalumu cha wakati bila kujali mabadiliko yake yanayotokea.
Katika Isimu daikronia, lugha huchunguzwa katika mtazamo wa historia ya mabadiliko yake. Hapa wanaisimu hulinganisha lugha kwa kuangalia tofauti zake zinazotokana na mabadiliko ya kihistoria na kuzielezea tofauti hizo. Kwa mfano mabadiliko yaliyoko kati ya Kiswahili cha kale mathalan enzi za miaka ya 1900 na Kiswahili cha sasa yanawezwa kuelezewa kifonolojia, kisarufi, na kimaana.
Umilisi (langue) na Utendi (parole)
Umilisi ni ujuzi alio nao mjua lugha kuhusu lugha yake. Ni ujuzi alio nao mjua lugha ambao upo katika ubongo wake. Ujuzi huo huhusu kanuni zinazotawala lugha hiyo husika. Kwa mujibu wa Rubanza 2003, ujuzi huu humwezesha kutambua sentensi sahihi, zisizo sahihi na kupambanua sententi zenye utata. Ujuzi huo humwezeha kupuuza makosa ya kiutendaji katika mazungumzo kama vile kuteleza kwa ulimi, kukatisha sentensi.
Baruapepe ya mwandishi: [email protected]
Marejeo
Msanjila, Y. P. (1990). “Problems of Teaching Through the Medium of Kiswahili in Teacher Training Colleges in Tanzania”. Journal of Multilingual and Multicultural Development II/4:307 – 318
Mtembezi, I. J. (1997). “Njia Mbili Zilimshinda Fisi: Tanzania na Suala la Lugha ya Kufundishia”. Dar es Salaam: BAKITA.
Mulokozi, M. M. (1991). “English versus Kiswahili ni Tanzania’s Secondary Education”. Swahili Studie Ghent.