Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Nimeolewa na mwanamume bure kabisa, hashughuliki nyumbani, kila jukumu aniachia
Wanandoa wanaofarakana kwa sababu ya mchezo wa huba. Picha|Maktaba
SWALI: Hujambo shangazi. Nimeolewa kwa miaka minne lakini kila jukumu liko mabegani mwangu, iwe ni kodi, chakula, ada ya watoto. Mume wangu husema mwanaume si ATM. Je, niendelee kuvumilia au nichukue hatua?
Jibu: Ni kweli mwanaume si ATM, lakini pia hafai kuwa mzigo. Ndoa ni ushirikiano wa majukumu. Kama mzigo uko upande mmoja, kuchoka ni lazima. Kaa chini mzungumze, weka mipango ya kifedha. Kuvumilia bila suluhu ni kujiumiza polepole.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO