Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Tumehusiana miaka 7 bila kupelekwa kwao
Picha ya wapenzi wawili baada ya ugomvi. Picha| Maktaba
SWALI: Vipi shangazi. Tumekuwa kwenye uhusiano miaka saba lakini mpenzi wangu hajawahi kunipeleka kwao. Anasema bado anajiandaa. Niendelee kusubiri?
Jibu: Miaka saba ni muda wa kutosha wa kujua unachotaka. Kama bado hajawa tayari, huenda tatizo si muda bali nia. Usikae kwenye uhusiano ukisubiri bila mwelekeo.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO