• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
WASONGA: NCPB na HELB zianze miradi mbadala ya kujichumia fedha

WASONGA: NCPB na HELB zianze miradi mbadala ya kujichumia fedha

Na CHARLES WASONGA

BODI ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB) na ile ya Kutoa Mikopo ya Kufadhili Elimu ya Juu (HELB) ni asasi zinazotekeleza wajibu mkubwa na muhimu zaidi kwa Wakenya.

NCPB hununua nafaka kwa niaba ya serikali kupitia maghala yake yaliyoko maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, katika kipindi cha miaka kadha iliyopita, bodi hii imekuwa ikiuza mbolea kwa wakulima chini ya mpango wa kuwasilisha bidhaa hiyo kwa bei nafuu; ya Sh1,800 kwa gunia moja la kilo 50.

Hata hivyo, mwaka huu serikali kuu ilifutilia mbali zabuni ya uagizaji mbolea ikidai inahitaji muda kulainisha shughuli hiyo ili kuzima mianya iliyotumiwa na walaghai kuingiza mbelea feki.

Hatua hii inaashiria kuwa katika msimu huu wa upanzi wa mahindi, wakulima wataathirika pakubwa kwani watalazimika kununua mbolea hiyo kwa bei ghali kutoka kwa wauzaji reja reja.

Baadhi ya wakulima wanauziwa bidhaa hii kwa kati ya Sh3,500, bei ambayo imewalemea baadhi yao wenye mapato ya chini.

Na HELB inakabiliwa na changamoto si haba katika utekelezaji wajibu wake wa kuwapa wanafunzi mikopo kwa sababu wengi wa waliofaidi miaka ya nyuma wamedinda kulipa.

Hii ndio maana wiki jana Waziri wa Elimu Amina alisema serikali itatumia polisi kuwasaka watu hao ambao wanadaiwa jumla ya Sh7.2 bilioni na bodi hiyo.

Kwa hivyo, ushauri wangu ni kwamba NCPB na HELB zinapaswa kukoma kutegemea ufadhili kutoka kwa serikali kuu, ili ziweze kuendelea kutekeleza majukumu yao bila tatizo.

Wabunge na maseneta waandae miswada ya kubadili sheria za bodi hizi ili ziweze kuwa na uwezo wa kushiriki shughuliza za uzalishaji mapato ya kufadhili shughuli zake.

Kwa mfano, bodi hizi zinaweza kuwekezaji pesa ambazo huchuma kila mwaka kutoka kwa huduma kwa wateja wao, vianzo vinginevyo, kuanzisha miradi ya ujenzi wa majumba ya kukodisha.

Mradi kama huu umekuwa ukiendeshwa na Hazima ya Malipo ya Uzeeni (NSSF) na kampuni kadhaa za bima.

Ikiwa HELB inakuwa na miradi mbadala ya kuiingizia mapato nadhani ingepunguza hii hali ya sasa ambapo inategemea ufadhili kutoka kwa serikali kuu na fedha kutoka wale ambao walifaidi kwa mikopo yao miaka ya nyuma.

Na ikiwa NCPB ingekuwa imeanzisha miradi mbadala ya kuiletea hela kama vile kiwanda cha kutengeneza mbolea au kutoa bima kwa wakulima ingeweza kuwalipa wakulima na kuwauzia mbolea kwa bei nafuu badala ya kutegemea kudura za serikali ya kitaifa.

You can share this post!

ULAGHAI: Gakuyo alivyotumia injili kuwapunja wawekezaji

Polo ajuta kujifanya dume la kupokonya wenzake mademu

adminleo