• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 1:14 PM
Riba ya ‘Okoa Jahazi’ ya Safaricom ni haramu, wananchi waambia mahakama

Riba ya ‘Okoa Jahazi’ ya Safaricom ni haramu, wananchi waambia mahakama

Na BERNARDINE MUTANU 

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu, Safaricom imo matatani baada ya kushtakiwa kuhusiana na moja ya huduma zake.

Kampuni hiyo ilishtakiwa Jumatatu na wananchi wawili kuhusiana na huduma yake ya ‘Okoa Jahazi’ ambayo walisema hutozwa riba waliyodai ni haramu.

Safaricom ilishtakiwa na Ashford Koome na Eric Kithinji, walidai kuwa kampuni hiyo haijapewa leseni ya kutoa huduma za benki, hivyo, riba wanayotoza huduma hiyo ilikuwa haramu.

Hata hivyo, kwa kujitetea, kampuni hiyo ilisema hiyo ni ada na sio riba kama walivyodai, kwa kuwa imeidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (CA).

Safaricom ndiyo kampuni inayopata faida kubwa zaidi kati ya kampuni zote nchini Kenya kwa mwaka. Ina watumizi wengi zaidi wa huduma zake za kupiga simu, kutuma arafa, M-Pesa, M- Shwari, Bonga points na Okoa Jahazi.

Kampuni zingine za mawasiliano Airtel na Telkom pia zina huduma za kukopa hela za kutumia kwa simu, lakini ile ya Safaricom ndiyo hutumiwa na wananchi wengi nchini.

You can share this post!

Singapore kuwapa raia wake hela za bwerere

iHub yazindua vituo vya uvumbuzi Marsabit na Garissa kuokoa...

adminleo