• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 7:50 AM
Havi hajahitimu kuwania urais LSK – Mahakama

Havi hajahitimu kuwania urais LSK – Mahakama

Wakili Nelson Havi. Picha/ Maktaba

Na RICHARD MUNGUTI

NDOTO za wakili Nelson Havi kuwa rais wa Chama cha Wanasheria nchini (LSK) ziliambuliwa patupu Jumanne wakati mahakama ya rufaa ilipomtangaza hajahitimu.

Mahakama hiyo ya pili kwa ukuu nchini ilisema sheria za LSK zasema rais wake sharti awe ametekeleza majukumu ya uwakili kwa miaka 15.

Ombi hilo lilikuwa limewasilishwa na wakili Nelson Andayi Havi akitaka akubaliwe kuwania urais wa chama hicho.

Bw Havi amefungiwa nje kwani hajatimiza miaka 15 ya kuhudumu akiwa wakili kama sheria za LSK zinavyoeleza.

Akitupilia mbali kesi hiyo, Jaji John Mativo alisema LSK hakikukosea kilipokataa kuchapisha jina la Bw Havi kwenye karatasi za kura.

Urais wa chama cha LSK umevutia mawakili wa tajriba ya juu akiwamo aliyekuwa Seneta mteule Judith Sijeni, aliyekuwa rais wa chama cha mawakili Afrika Mashariki Aggrey Mwamu na Bw Allan Waiyaki.

You can share this post!

Shehe kusalia ndani kuhusu ugaidi

Nuttal apigwa kalamu Ghana kuhusu ufisadi

adminleo