Kijana aliyetoroka Al Shabaab asimulia maisha yalivyokuwa akiwa gaidi

Na MOHAMED AHMED

Kwa Muhtasari:

 • Kijana huyo amekuwa akiishi maisha ya kisiri ili maafisa wa usalama ama wafuasi wa Al Shabaab wasimtambue
 • “Nilimtembelea binamu yangu Lamu na kuishi kwake kwa miezi mitatu. Baadaye alinijulisha kwa vijana wengine watatu kisha akatupa Sh10,000 kila mmoja”
 • “Tulifika kwenye kambi iliyokuwa na vijana wapatao 200. Hapo ndipo nilipong’amua kuwa nilikuwa ndani ya kambi ya Al Shabaab nchini Somalia”
 • Mafunzo yalihusisha jinsi ya kutumia silaha tofauti kama bunduki, gurunedi miongoni mwa nyingine. Pia tulibebeshwa magunia mazito yaliyojaa mchanga
 • “Singeweza kuvumilia tena. Mwezi moja baada ya kugombana na kamanda, nilipanga na Mkenya mwingine jinsi tungehepa”

VIJANA wanaorudi nchini baada ya kuhepa Al Shabaab nchini Somalia wanajutia kwa kujiunga na kundi hilo la kigaidi.

Majuto yao yanatokana na kuwa hawawezi kuishi maisha ya kawaida kwa hofu ya kuwindwa na polisi ama kuuawa na wafuasi sugu wa kundi hilo ambalo limetatiza usalama hasa kaunti za Lamu, Wajir na Mandera.

Taifa Leo ilikutana na mmoja wa vijana hao, ambaye ni kijana wa miaka 29 katika kaunti ya Kwale aliyerudi nchini 2015.

Kijana huyo amekuwa akiishi maisha ya kisiri ili maafisa wa usalama ama wafuasi wa Al Shabaab wasimtambue. Tulipomtembelea nyumbani kwao, mwanzo alikataa kuzungumza nasi kwa kuhofia kuwa tulikwa makachero. Lakini alikubali tulipomhakikishia kuwa sisi ni wanahabari:

“Safari yangu ya kujiunga na Al Shabaab ilianza 2014. Binamu yangu alinialika Lamu kwa ahadi kuwa ningepata kazi nzuri. Alifahamu kuwa nilikuwa nafanya vibarua hapa na pale licha ya kuhitimu katika Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS). Aliniambia ningeajiriwa kazi yenye malipo mazuri.

Nilimtembelea binamu yangu Lamu na kuishi kwake kwa miezi mitatu. Baadaye alinijulisha kwa vijana wengine watatu kisha akatupa Sh10,000 kila mmoja. Alitwambia tuingie gari la kibinafsi tupelekwe mahala ambapo tungeanza kufanya kazi aliyokuwa ameahidi ambapo tungelipwa Sh40,000 kwa mwezi.

 

Mafunzo ya miaka miwili

Tulifika kwenye kambi iliyokuwa na vijana wapatao 200. Hapo ndipo nilipong’amua kuwa nilikuwa ndani ya kambi ya Al Shabaab nchini Somalia. Humo kambini tulianza kupokea mafunzo ya kijeshi ambayo yalikuwa yachukue miaka miwili. Baadaye tungetumwa uwanja wa vita kupigana.

Mafunzo yalikuwa makali sana. Tulikuwa tukiamka saa kumi alfajiri ambapo tulishiriki mafunzo na mazoezi hadi saa kumi na moja jioni.

Mafunzo yalihusisha jinsi ya kutumia silaha tofauti kama bunduki, gurunedi miongoni mwa nyingine. Pia tulibebeshwa magunia mazito yaliyojaa mchanga. Ilikuwa ni lazima ushiriki mafunzo upende usipende.

Siku moja kamanda aliniagiza ninyanyue gunia la kilo 50 la mchanga lakini nikateta. Alichomoa kisu kwa nia ya kunidunga. Nilishika kisu hicho kikanijeruhi mkono wa kushoto. Hivyo ndivyo nilivyopata jereha hili mkononi ambalo hunikumbusha masaibu niliyopitia mikononi mwa Al Shaabab.”

Majonzi yalivyokumba kijiji cha Malili, Witu kaunti ya Lamu Agosti 2017 baada ya wanakijiji kuuawa na magaidi wa Al Shabaab. Polisi wamehusisha baadhi ya vijana waliojiengua kwa kundi hilo na mashambulio yaliyofanyika Kwale. Picha/ Maktaba

Alivyohepa

“Singeweza kuvumilia tena. Mwezi mmoja baada ya kugombana na kamanda, nilipanga na Mkenya mwingine jinsi tungehepa. Ilikuwa Agosti, 2015 ambapo tulitoroka usiku na kuanza kutembea tukiwa na imani tungefika Kenya.

Tulifahamu kuwa hatua hiyo ilikuwa hatari kwani tungeweza kuuawa na wenzetu wa Al Shabaab ama maafisa wa usalama. Lakini tuliamua heri tufe tukitafuta uhuru wetu badala ya maisha ndani ya Al Shabaab.

Baada ya kutembea kwa siku mbili msituni tulipatana na mzee ambaye alitusaidia kufika Mandera. Kisha tuliingia lori lililotupeleka Garissa. Mjini Garissa tulipanda basi lililotupeleka Mombasa kisha mimi nikaja hapa nyumbani naye mwenzangu akaenda kwao Kilifi.

Watu hapa kijijini hawashuku hata kidogo kuwa nilikuwa nimejiunga na Al Shabaab. Niliingizwa katika kundi hilo bila kufahamu. Tangu niliporudi nimekuwa nikiishi maisha ya utulivu na familia yangu. Kinyume na wengine wanaorudi, mimi sitaki kujiingiza katika uhalifu.”

 

Habari zinazohusiana na hii

Comments

 • Anonymous

  03/19/2020

  achene mchezo

 • Gilbert Lewandoski

  02/19/2020

  hiyo ni kazi nzuri kutoka Al-shaabab si kazi rahisi

 • ladislaus colnel

  12/25/2019

  kweli ila umezingua kuwah kulud ungesubili ujifunze zaidi ili uwe na uwezo wa kuteka hata maisha yakiwa magumu

 • Patrick Mwandikwa

  12/18/2019

  wewe wafaa kugiunga na jesi ya kenya ili kuwangamiza ao magaidi bwana any kazi nzuri

 • Dhhdhd

  12/16/2019

  Bro ulikua ubaki kama miaka 4 ivi kenya utakufa maskini

 • Abrahams K Kirianki

  12/16/2019

  Swadakta kabisa kwa kazi nzuri

 • dege

  08/17/2019

  mimi nahisi ungestahamili kwanza kwa muda kama mwaka mmoja ili upate mafunzo .umefanya haraka sana kutoroka.

 • Anonymous

  08/01/2019

  asante kwa kuepuka kifo na kuwaelimisha vijana wengine

 • Anonymous

  02/23/2019

  Nayo kuna al-shabaab ndani ya kenya? Swali langu ni hili mbona pokot wanafamia county yenye ni jirani yao?jua pokot wanataka vita xo serikali waongeleshe vizuri pokot.

 • EVANS KIRWA

  02/21/2019

  ASANTE KWA KAZI NZURI

 • dicklack

  02/16/2019

  axante qwa kuepuka kifo

 • Juma Mutiatiaki Dominic

  02/11/2019

  Hongera

 • Anonymous

  01/25/2019

  Wekeni share ya whatsapp wengine tunatumia whatsapp hatutumii twittter wala facebook

 • kara

  01/23/2019

  ai

 • Said Mwauchi

  01/21/2019

  Asante Kwa Kazi Nzuri

 • Weikwe Peter

  12/28/2018

  Tutawafanyia Maombi Kwa Maulana

 • njuguna chege

  11/27/2018

  please choose friends wisely

 • JANE AMREAL

  11/19/2018

  gov’ inafaa iwasaidie mayut with jobs na iwasaidia kuinua talanta

 • Anonymous

  10/19/2018

  kenya ibuni nafasi za jazi kwa vijana ili waache tamaa.

 • bint mwagasare

  10/16/2018

  that is great

 • Kijana mdogo wa Navakholo

  10/14/2018

  Watolewe huko haraka!

 • gabriel javan

  08/17/2018

  its hard,,,but try your best

 • nicholas-jhons

  05/07/2018

  ninajambo ningependaniponge nasrkali sijuikamanaeza patanafasi kamamnawesapasikunisaitia nipigieni simu hapa

 • MOROTI

  03/19/2018

  ASANTE KWA KAZI NZURI

Leave a Reply