Makala

TAHARIRI: Agizo la Rais kuhusu ufadhili litekelezwe

March 16th, 2019 Kusoma ni dakika: 2

Na MHARIRI

AGIZO la Rais Uhuru Kenyatta kwamba timu zote za kitaifa zitakazowakilisha Kenya katika mashindano ya kimataifa zifadhiliwe na serikali limeibua hisia mseto miongoni mwa wadau.

Akizungumza mwishoni mwa makala ya nne ya mbio za Beyond Zero Marathon wikendi jana, Rais aliwahakikishia wanamichezo kuwa serikali yake itafadhili vikosi vyote vitakavyowania mataji mbal- imbali katika majukwaa ya kimataifa.

“Michezo na sanaa ni sehemu muhimu ya utamaduni wetu. Ni sekta ambayo haiwezi kabisa kuachwa mikononi mwa wahisani pekee,” akatanguliza.

“Mwaka 2019, Harambee Stars haitaomba wala kukopa fedha. Itafadhiliwa kikamilifu na serikali. Timu za taifa za raga, voliboli, mpira wa pete na nyinginezo zote zitafadhiliwa kikamilifu na serika- li,” akaongeza Rais Kenyatta na kusisitiza kwamba wanariadha pia watafadhiliwa na hawatakosa sare wala viatu kila watakapokuwa wakipeperusha ben- dera ya Kenya katika mashindano ya kimataifa.

Agizo hilo la Rais linatolewa wakati ambapo Wizara ya Michezo bado inajizatiti kuhakikisha kwamba mashirikisho yote ya michezo yanazingatia Sher- ia za Michezo zilizopitishwa na Bunge mnamo 2013.

Ni chini ya sheria hiyo ambapo Hazina ya Michezo ilibuniwa kwa lengo la kuimarisha miundombinu, ujenzi wa miundo-misingi na kuboresha maslahi ya wanamichezo.

Kwa mujibu wa Richard Omwela ambaye ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Raga (KRU), agizo la Rais litachangia pakubwa katika ufufuo wa kikosi cha Shujaa ambacho kimeshuka pakubwa kimataifa.

Mbali na kuvuta mkia katika duru ya Vancouver Sevens nchini Canada wikendi jana, Shujaa wal- iteremka hadi nambari 14 baada ya kupoteza mechi tano mfululizo kwa kupepetwa 47-7 na Australia ka- tika robo-fainali ya Challenge Trophy na 22-14 dhidi ya Japan katika nusu-fainali ya kutafuta mshindi wa nambari 13 hadi 16.

Awali walizabwa na Fiji (36-12), Samoa (35-12) na Canada (36-21) mechi za makundi.

Kwa pamoja na kocha Paul Murunga, Omwela anaamini kwamba mchango wa serikali utapigisha Shujaa hatua zaidi katika kampeni za duru zijazo za Hong Kong (Aprili 5-7), Singapore (Aprili 13-14), Uingereza (Mei 25-26) na Ufaransa (Juni 1-2).

Kenya imekuwa moja ya timu zinazoshiriki duru zote kwa misimu 16 mfululizo tangu 2002-2003.

Ingawa hivyo, imekuwa ikining’inia padogo msimu huu baada ya wachezaji wazoefu kugoma wakilalamikia kupunguziwa mshahara.

Kwa upande wake, Nick Mwendwa ambaye ni Rais wa Shirikisho la Soka (FKF), amesema serikali bado haijajibu ombi lao la kuwasafirisha wanaso- ka wa Harambee Stars wanaochezea ng’ambo kwa mechi ijayo dhidi ya Ghana.

Ratiba Stars wameratibiwa kuchuana na Ghana katika mchuano wa mwisho wa Kundi F wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Afrika (AFCON) zitakazoandal- iwa nchini Misri kati ya Juni 21 na Julai 29.