• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 11:05 AM
Tumbojoto polo kuambia jaji ampunguzie kifungo kama walivyoelewana

Tumbojoto polo kuambia jaji ampunguzie kifungo kama walivyoelewana

NA PHYLIS MUSASIA

NAKURU MJINI

POLO wa hapa alishangaza mahakama alipomwambia jaji abatilishe hukumu ya miaka 75 hadi 25 walivyokuwa wameelewana awali.

Jamaa alisingizia hayo baada ya mahakama kukataa rufaa yake na kudumisha hukumu aliyopewa kwa unajisi.

Hata hivyo, jaji alitaka kujua ni lini na wapi wawili hawa walizungumzia kuhusu kubatilishwa kwa hukumu hiyo.

Mwanamume huyo alikuwa amepatikana na hatia ya kuwanajisi wasichana watatu siku tofauti katika kijiji kimoja katika Kaunti ya Nakuru.

Punde baada ya kupewa adhabu hiyo alimuuliza jaji iwapo alikuwa amesahau maafikiano yao.

Hakimu alishtuka na kumuuliza walikuwa wamekutana wapi na walikubaliana nini.

“Eleza mahakama kinagaubaga ni lini mimi na wewe tulikaa chini tukazungumza kuhusu kubatilishwa kwa hukumu uliyopokezwa au chochote kile,” jaji alimwambia.

Kalameni huyo alikuwa amekata rufaa dhidi ya hukumu ya miaka 75 aliyopokezwa kama adhabu ya makosa aliyotenda lakini rufaa hiyo ilitupiliwa mbali kwa kukosa msingi.

“Yafaa uelewe kuwa hapa ni mahakamani na kwamba huu si mchezo wa kandanda kati ya Man-U na Arsenal. Itakuwa ni vyema ikiwa utafuata sheria na kutii uamuzi wa korti na ikiwa bado una tashwishwi basi kunazo njia mwafaka za kufuata,” jaji alimkanya polo huyo.

Hata hivyo, jombi huyo aliendelea kutilia mkazo ombi lake huku akitaka apunguzizwe adhabu hiyo.

“Tayari nimeshakaa jela kwa muda kiasi cha haja na nimeonelea itakuwa vyema korti ikinionea huruma na kunipunguzia miaka niliyofungwa jela,” alisisitiza polo huyo.

llibidi afisa wa jela aingilie kati na kumuinua juu juu kalameni huyo hadi seli baada ya jaji kuamuru aondolewe kwa kusababisha utata kortini.

 

You can share this post!

Joho na Kingi sasa waombwa kuungana kabla ya 2022

WASONGA: Tujikakamue kama nchi kumaliza aibu ya raia kufa...

adminleo