• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 9:35 PM
ULIMBWENDE: Faida za manjano (turmeric) katika urembo

ULIMBWENDE: Faida za manjano (turmeric) katika urembo

Na MARGARET MAINA

MANJANO ni kiungo kinachotokana na mti uitwao Curcuma longa.

Mti huu unapatikana sana Kusini mwa Bara Asia.

Kiungo hiki kinatumika sana katika upishi kuongeza ladha kwenye vyakula, lakini pia htumiwa kwa urembo.

Faida za manjano ikitumika kwenye ngozi

Manjano ina ufanisi mkubwa kwa kazi ya kutibu chunusi kwa sababu ina ‘antiseptic’ na ‘antibacterial’ ambazo husaidia kupambana dhidi ya chunusi na vidonda usoni na kuipa ngozi mwonekano mzuri.

Manjano pia husaidia kupunguza mafuta usoni kwa wale wenye nyuso zenye mafuta.

Vinavyohitajika

–          Liwa kijiko 1 cha chai

–          Manjano kijiko 1

–          Juisi ya limau kiasi

Changanya viungo hivi pamoja na kisha upake usoni na ukae navyo kwa muda usiopungua dakika 10.

Manjano. Picha/ Hisani

Kwa kuondoa chunusi, changanya manjano na maji safi kisha paka usoni na ukae hivyo kwa robo saa kabla ya kunawa uso wako kwa maji fufutende

Barakaoa (mask) kwa wenye nyuso za mafuta

Manjano huwa na manufaa katika ngozi zenye mafuta na husaidia kupunguza mafuta na hiyo bila shaka husaidia kupunguza chunusi usoni.

Vinavyohitajika

–          juisi ya machungwa

–          liwa

–          manjano

Vichanganye vyote hivyo. Paka mchanganyiko usoni na ukae nao kwa dakika 10-15 kisha baadaye unawe uso wako.

Mask kwa ngozi kavu

Kama una ngozi kavu, unaweza kutengeneza mask kwa kuchanganya ute wa yai moja, mafuta ya mizeituni vijiko viwili vya chai na manjano vijiko viwili.

Mchanganyiko huu unaweza kuutumia kwenye ngozi kavu kama vile usoni, shingoni, magotini. Ni muhimu uuache kwa kati ya dakika 15-20 kabla ya kunawa.

Huondoa makunyanzi

Manjano ikichangaywa pamoja na viungo vingine ina ufanisi katika kuondoa makunyanzi usoni.

Unaweza kuandaa mchanganyiko kwa kuchanganya unga wa manjano pamoja na unga wa mchele, maziwa na juisi ya nyanya na kupaka usoni na shingoni, kisha ukae kwa muda wa nusu saa kabla ya kunawa kwa maji fufutede.

Ukifanya hivi angalau mara moja kwa wiki, bila shaka utaanza kuwa na uso unaong’aa na kupendeza ajabu!

Kuondoa michirizi (stretchmarks)

Manjano husaidia kufuta michirizi.

Changanya manjano na maziwa au maji kisha upake kwenye eneo ngozini palipo michirizi. Baada ya nusu saa hivi, oga kwa maji fufutende kisha ujipake losheni.

Faida za manjano kwenye nywele

Manjano husaidia katika ukuaji wa nywele, pia kuondoa mba. Changanya manjano na olive oil, kisha paka kichwani na ukae hivyo kwa nusu saa kabla ya kuoga.

Mchanganyiko huu ukiongezwa asali pia hupunguza kero ya kukatika kwa nywele.

You can share this post!

KULEA VIPAJI: Klabu ya Ngoingwa FC

Pipeline yaondolea Kenya aibu kipute cha voliboli Misri

adminleo