Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Nafasi ya lugha rasmi katika jamii

April 10th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MARY WANGARI

LUGHA rasmi ni lugha inayotumiwa katika shughuli za kiserikali kama vile bungeni, mahakamani, utawala, elimu na maeneo mengineyo.

Ni lugha iliyotwikwa jukumu la kutumika kikazi.

Sifa za Lugha Rasmi

  1. Lugha rasmi inaweza kuwa lugha mojawapo ya wenyeji au lugha ya kigeni. Kiswahili kama lugha ya wenyeji katika mwambao wa Afrika Mashariki kinatumika kama lugha rasmi nchini Kenya na Tanzania.
  2. Sifa kuu ya lugha rasmi ni kwamba inatambulika na serikali tawala kwa kuwa ni sharti itumike katika shughuli rasmi na kutekeleza majukumu ya serikali.
  3. Ina sifa ya kuwa na msamiati tosha wa kisayansi na kiufundi. Hata hivyo, kuna baadhi ya lugha rasmi ambazo hazina msamiati tosha wa sayansi na ufundi.
  4. Lugha rasmi inaweza kutumiwa katika kiwango cha kitaifa na kimataifa. Nchini Kenya na Tanzania, Kiingereza na Kiswahili ni lugha rasmi katika kiwango cha taifa na kimataifa.
  5. Si lazima iwe na wazungumzaji wengi katika nchi husika.
  6. Inaweza kutekeleza majukumu mengine licha ya kuwa lugha rasmi. Kwa mfano, nchini Tanzania na Kenya, Kiswahili kinatumika kama lugha rasmi na lugha ya taifa. Si lazima iwe na wazungumzaji wengi katika nchi husika.
  7. Inaweza kutekeleza majukumu mengine licha ya kuwa lugha rasmi.Mathalani nchini Tanzania na Kenya, Kiswahili kinatumika kama lugha rasmi na lugha ya taifa.
  8. Aghalabu, lugha rasmi huwa ni lugha yenye historia ndefu ya maandishi.
  9. Huwa imesanifishwa na kusambazwa kupitia vyombo vya habari, vitabu na machapisho mengine.

Lugha rasmi hutekeleza majukumu yafuatayo katika jamii

  1. Hutumika kuendesha shughuli zote katika ofisi za serikali.
  2. Kufundishia kutoka shule za msingi hadi vyuo vikuu.
  3. Hutumika katika hati zote za serikali.

 

[email protected]

Marejeo

Chiraghdin, S., Mnyampala, M. (1977). Historia ya Kiswahili. Nairobi: Oxford University Press.

Richards, J.C., (1984). Error Analysis Perspectives on Second Language Acquisition. London: Longman Group Ltd.

Wardhaugh, R., (1986). An Introduction to Socio-Linguistics. New York: Blackwell Publishers.