Dondoo

Demu ahepa na long'i ya polo lojing’i

April 11th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na John Musyoki

ELDORET MJINI

JAMAA mmoja mjini hapa alibubujikwa na machozi demu alipokataa katakata kumpa suruali yake wakiwa lojingi baada ya kuburudishana.

Penyenye za mtaani zinasema jamaa alikataa kumlipa demu naye akachomoka chumbani na long’i yake.

Duru zinasema jamaa alipiga nduru demu alipotoka nje na long’i yake.

“Kujeni wahudumu wa lojingi hii. Huyu demu anaondoka na long’i yangu. Jameni nisaidieni,” jamaa alisikika akipiga nduru.

Demu aliposimamishwa na wahudumu wa lojing’i alidai jamaa alikataa kumlipa baada ya kumburudisha na alitaka amlipe haki yake kwanza kabla ya kumpa long’i hiyo.

“Huyu jamaa ni fala sana, baada ya kumburudisha amekataa kunilipa pesa zangu zote. Amenipa Sh250 badala ya 700. Simpi long’i mpaka atakapolipa peza zangu zote,” demu alisikika akiwaambia wahudumu.

Yadaiwa jamaa alimsihi demu ampe suruali yake naye akakaa ngumu. “Tafadhali usiende na lon’gi yangu. Nipe muda niende ATM nitakuongezea pesa zako. Sikuwa na zingine,” jamaa alimwambia demu.

Licha ya jamaa kulia, dua zake ziliambulia patupu. Demu alipiga hatua na kuondoka huku watu wakiangua vicheko. Wahudumu walimsihi demu ampe jamaa long’i yake lakini demu hakuwasikiliza.

“Tunakusihi umpe long’i yake tu huenda hakuwa na pesa zingine,” mhudumu mmoja alisikika akimwambia demu.

Hata hivyo demu aliwasuta. “Sitaki kisirani chenu nyinyi. Shauri yake, kwa nini alinidanganya. Akiongeza pesa nitampa long’i yake. Anipigie simu nimletee long’i yake akipata pesa. Mimi sipendi watu kisirani,” demu alifoka na kuondoka.

Kwa upande wa jamaa alijikunyata mle chumbani kama kuku aliyenyeshewa. Haikujulikana iwapo demu alirejea baadaye na kumpa jamaa long’i yake.