MAPISHI: Queencakes zikiwa na ndizi
Na MARGARET MAINA
MUDA wa kuandaa: Dakika 10
Muda wa kuoka: Dakika 40
Walaji: 4
Vinavyohitajika
– Unga wa ngano vikombe 2
– Baking soda kijiko 1
– Baking powder kijiko 1
– Chumvi ½ kijiko
– Ndizi 3 kubwa zilizoiva vizuri
– Buttermilk vijiko 3
– Maziwa vijiko 3
– Yai 1
– Vanilla ¼ kijiko
– Nutmeg ½ kijiko
– Sukari ¾ kikombe
– Mdalasini ¼ kijiko
– Butter vijiko 5 au Blueband
Maelekezo
– Pasha ovena nyuzijoto 190°C,
– Chukua bakuli, weka unga, baking soda, baking powder, chumvi, nutmeg kisha changanya vizuri
– Yeyusha siagi. Menya ndizi na uvikate vipande vidogo vidogo,ongeza sukari, maziwa, buttermilk na yai kisha anza kuziponda.
– Ongeza siagi na uchanganye vizuri.
– Chukua mchanganyiko wenye ndizi changanya kwenye ule wenye unga, kisha anza kukoroga uchanganyikane wote kwa pamoja.
– Kisha chukua bakuli lingine, weka sukari vijiko viwili vya chai, unga vijiko viwili vya chakula, mdalasini na butter changanya vizuri.
– Kisha weka mchanganyiko huo kwenye mchanganyiko ule wa unga.
– Tumia kijiko kuweka mchanganyiko kwenye karatasi ya queencakes
– Kisha weka kwenye chombo cha kuokea na uoke kwa dakika 40
– Ikishakuwa na rangi ya kahawia, epua.
Acha vipoe kabla ya kupakua na juisi au maziwa.
Furahia.