• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 6:55 PM
ULIMBWENDE: Jinsi ya kuondoa weusi chini ya macho

ULIMBWENDE: Jinsi ya kuondoa weusi chini ya macho

Na MARGARET MAINA

[email protected]

KULALA kwa maana ya kupata usingizi wa kutosha na kupumzika ni muhimu kwa kuwa huchangia mtu kuwa na afya nzuri na mwonekano mzuri.

Hata hivyo, sio rahisi kuupata usingizi wa kutosha kila usiku na wakati mwingine inaonyesha usoni – chini ya macho hasa – mtu anapokuwa hajalala vizuri ambapo anakuwa na ‘puffy eyes’.

Viazi

Viazi vina asili ya enzymes zinaong’arisha ngozi, ambazo husaidia kufifisha weusi chini ya macho.

Weka kiazi kibichi katika hiyo sehemu ya macho. Unaweza kukata vipande vidogovidogo na vyembamba au kwa kusaga kupata rojo. Weka kwa nusu saa kabla ya kutoa na kutumia kuosha uso kwa maji ya ufufutende.

Majani ya mint 

Yaponde majani ya mint kidogo na paka machoni hapo kwa dakika tano. Osha uso kwa maji ya kawaida. Unaweza kutumia majani ya mint ukachanganya na asali au mafuta ya mizeituni, olive oil, kabla hujapaka sehemu ya macho. Baada ya kuosha, paka ‘moisturizer’.

Tea bags

Caffeine iliyoko ndani ya majani chai ina uwezo wa kukazisha ngozi chini ya macho na pia huondoa kuungua na mbadiliko wa rangi. weka tea bags mbili kwenye maji kisha yaweke kwenye macho yako yakiwa yamefungwa kwa kuilaza kwa dakika 15.

Rose water

Rose water huwa na vitamini kama A na C, na antiseptiki. Unapaswa kuyapaka hayo maji chini ya macho kwa dakika 10 kwa kutumia pamba.

Matango

Kuweka vipande vya matango ya baridi kwenye kila jicho husaidia kuondoa uchovu na husaidia kulainisha ngozi ya machoni. Matango pia hufanya kazi ya kukaza na kung’arisha uso, vilevile husaidia kuondoa mabadiliko ya rangi katika ngozi.

You can share this post!

WAKILISHA: Atumia Hip hop kuongoa vijana

SWAGG: Emily Bett

adminleo