• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 6:27 PM
Baba Yao awataka waliomkaanga kuhusu bajeti wamuombe radhi

Baba Yao awataka waliomkaanga kuhusu bajeti wamuombe radhi

Na PETER MBURU

GAVANA wa Kiambu Ferdinand Waititu sasa anawataka watu wote waliokuwa wakimkashifu kuhusiana na ripoti kuwa serikali ya kaunti yake ilitumia mamilioni ya pesa kufadhili miradi ya kitaifa na kimataifa kumuomba msamaha.

Hii ni baada ya kuibuka kuwa si Kaunti ya Kiambu pekee ambapo kulingana na jinsi bajeti zilitumiwa serikali ya kaunti ilitumia ilifadhili miradi ya serikali kuu, ila katika kaunti zingine.

Jumatatu, ilibainika kuwa kaunti za Kakamega, Nyeri, Kitui na Samburu pia zilikuwa na utata katika bajeti zake.

Tangu wiki iliyopita, Gavana Waititu amekuwa kikaangoni kuhusiana na ufichuzi kuwa kaunti yake ilitumia mamilioni ya pesa kugharamia miradi ya utafutaji amani Sudan Kusini, mfumo wa shule za msingi bila malipo na kugharamia shughuli za ikulu.

Lakini baada ya kubainika kuwa huenda ni kosa la afisi zinazohusika na mambo ya bajeti, Bw Waititu amesema “Mkaguzi Mkuu angekuwa amejitokeza na kusema palipo na makosa. Ni bahati tu kuwa hali sawa imegunduliwa katika kaunti zingine.”

Akinyesha kupumua angalau kidogo, Gavana huyo ambaye alitetewa na Naibu Rais Jumapili alisema “Watu wote ambao walikuwa wakinikashifu sasa waniombe msamaha.”

Baadhi ya wakazi wa Kiambu tayari walikuwa wameanza kutoa wito kuwa gavana huyo ajiuzulu, baada ya Kamati ya Uhasibu katika Bunge la Seneti kumtaka kueleza ni vipi matumizi ya aina hiyo yalipatikana katika bajeti ya kaunti yake.

You can share this post!

Vifo kutokana na ajali vyaongezeka

Liverpool ina nafasi kutinga fainali UEFA, Daglish asema

adminleo