UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Motisha katika kusoma na kufundisha lugha mpya
Na MARY WANGARI
MOTISHA au ari inaweza kufafanuliwa kama tabia au msukumo katika kutimiza malengo fulani.
Kwa mujibu wa TUKI (2004), motisha inaelezwa kwamba ni kitu kama vile fedha inayotolewa ili kumtia mtu hamasa kujifunza jambo.
Hata hivyo, si lazima umpe mtu kitu bali unamtia moyo mwanafunzi na kumsaidia. Mwalimu anapaswa kutumia motisha chanya na wala sio motisha hasi. Kwa mfano hutakiwi kuchapa fimbo
Kwa mujibu wa Brown (1994), anafafanua motisha kama:
i. Kiwango cha uchaguzi ambacho unafanya kuhusu lengo unalotaka kufikia
ii. Jitihada atumiazo mtu kufikia malengo hayo
Kwa upande wao Skinner4 & Wattson wanaangazia zawadi na uhimizaji kwa wanafunzi pamoja na adhabu ili kufifisha na kujenga hali fulani.
Kuna aina mbalimbali za motisha jinsi tutakavyoziainisha ifuatavyo:
i. Mwamko au ari ya mwanagenzi binafsi
ii. Mazingira mazuri ya kufundishia Kiswahili kwa mfano, darasa, nje na kadhalika
iii. Jamii inayomzunguka ni motisha pia
iv. Mwalimu anaweza kuwa motisha kwa mwanafunzi
v. Zana au vifaa vya kujifunzia pia ni motisha
Je, umeipenda mada hii? Tuandikie maoni au wasiliana na mwandishi: [email protected]
Marejeo
Chiraghdin, S. & Mnyampala, M. (1977). Historia ya Kiswahili. Nairobi: Oxford University Press.
Richards, J.C. (1984). Error Analysis Perspectives on Second Language Acquisition. London: Longman Group Ltd.
Wardhaugh, R. (1986). An Introduction to Socio-Linguistics. New York: Blackwell Publishers.