• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 8:12 PM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Dhana ya motisha ikiwemo matawi yake katika lugha

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Dhana ya motisha ikiwemo matawi yake katika lugha

Na MARY WANGARI

YAPO makundi ya dhana ya motisha.

Motisha inajitokeza katika matawi mawili ambayo ni:

Motisha ya ndani

Motisha katika tawi hili haitegemei vitu vya nje ya yenyewe. Tawi hili la motisha linasimamia kile kinachoonekana kwa mwanagenzi wa lugha mwenyewe. Aidha, motisha katika tawi hili haibadiliki kulingana na muktadha wowote ule.

Motisha ya nje

Hii ni aina ya motisha ambapo mwanafunzi hutegema kupewa, kupata, kusikia au kuona.

Kundi hili la motisha humsaidia mwanagenzi katika kujifunza lugha. Ni muhimu kwa mwalimu kuwasaidia wanafunzi kujifunza lugha kulingana na muktadha husika.

Ili kufanikisha jambo hili ni sharti tuzingatie mambo haya muhimu:

Akili ya mwanafunzi – Ni sharti mwanafunzi aweze kutambua tofauti katika akili za wanagenzi wake ili kumwezesha katika shughuli ya kujifunza lugha.

Kipaji – Ni muhimu kwa wanafunzi kuzingatia vipaji vyao. Hii ni kwa kuzingatia uhalisia kwamba kuna baadhi ya wanafunzi waliojaaliwa vipaji vya kujifunza lugha.

Umri – Ni muhimu kukumbuka kwamba watu wazima huchelewa kujifunza lugha wakilinganishwa na watoto pamoja na vijana.

Jinsia – Aghalabu wanawake wanaweza kupata lugha haraka kuliko wanaume.

 

You can share this post!

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Motisha katika kusoma na...

OLUNGA ATUA: Olunga akamilisha kambi ya Harambee Stars...

adminleo