• Nairobi
  • Last Updated March 19th, 2024 1:13 PM
Rais wa CAF akamatwa kwa utoaji wa kandarasi ya Sh84.4 milioni bila kuhusisha maafisa wenzake

Rais wa CAF akamatwa kwa utoaji wa kandarasi ya Sh84.4 milioni bila kuhusisha maafisa wenzake

Na GEOFFREY ANENE na MASHIRIKA

RAIS wa Shrikisho la Soka barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad amekamatwa, tovuti ya Jeune Afrique nchini Ufaransa imeripoti Alhamisi.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, raia huyu wa Madagascar ametiwa nguvuni katika hoteli moja jijini Paris alikokuwa akiishi kwa ajili ya kongamano la 69 la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) lililofanyika Juni 5.

“Ahmad Ahmad alikamatwa Alhamisi asubuhi saa mbili unusu katika hoteli ya Berri jijini Paris kwa madai ya ufisadi na makosa ya kifedha,” tovuti hiyo inasema.

Habari zinasema kwamba kukamatwa kwake kunahusiana na utoaji wa kandarasi bila kuhusisha viongozi wengine alipokatiza kandarasi ya Puma kutoka Ujerumani na kupatia kampuni ya Technical Steel nchini Ufaransa.

Kusaini kandarasi, kulingana na katibu mkuu wa zamani wa CAF Amr Fahmy, kulikuwa na mapendeleo kutokana na urafiki kati ya Ahmad Ahmad na mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo ya Ufaransa, ambayo gharama yake itaongezeka na kufika Sh84.4 milioni.

Kongamano la FIFA lilishuhudia Rais wa FIFA, Gianni Infantino akihifadhi kiti chake.

You can share this post!

SHANGAZI AKUJIBU: Ataka nigharimie mahitaji yote na...

Mbwana Samatta ni andazi moto, amezewa mate na klabu nne za...

adminleo