• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 5:10 PM
MAPISHI: Namna ya kupika pilau yenye mboga tofauti

MAPISHI: Namna ya kupika pilau yenye mboga tofauti

Na: MARGARET MAINA

[email protected]

MUDA wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa kupika: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • Mchele wa kupikia biriani.
  • Bizari
  • Njegere
  • Majani ya giligilani
  • Kitunguu maji
  • Nyanya 3
  • Tangawizi 1
  • Vitunguu saumu 2
  • Viungo vya pilau
  • Karafuu
  • Pilipili
  • Pilipili mboga
  • Kolimaua
  • Karoti kiasi
Pilau yenye mboga tofauti. Picha/ Margaret Maina

Maelekezo

Menya vitunguu maji na kata kufuatisha uviringo wake ili upate umbo la mduara kisha weka kwenye chombo safi.

Osha nyanya na ukatekate vipande.

Osha karoti na kisha zimenye. Kwangua kiasi na zingine kata vipande vidogovidogo.

Osha kolimaua na njegere kwenye chombo chenye maji safi.

Menya tangawizi na vitunguu saumu kisha uvitwange.

Andaa viungo vyote vya pilau osha na kisha andaa karafuu na pilipili.

Weka mafuta ya kupikia kweye sufuria, yakishapata moto, weka viungo vya pilau vya unga kisha weka bizari na kaanga kwa muda kiasi.

Weka kitunguu saumu na ukoroge kiasi. Weka tangawizi na kitunguu maji kisha koroga. Acha viive kabla na kuanza kubadilika rangi.

Weka nyanya, chumvi, pilipili, karafuu, karoti, pilipili mboga, kolimaua na njegere. Endelea kukaanga kwa muda wa dakika kama 10.

Pilau yenye mboga tofauti. Picha/ Margaret Maina

Weka mchele huku ukiendelea kukaanga ili mchele wako uchanganyike vizuri na viungo kwenye sufuria.

Weka maji kulingana na kiasi cha mchele wako.

Weka moto wa wastani na kisha funika sufuria chakula kiive. Baada ya dakika 15, geuza pilau kisha weka majani ya giligilani na ufunike chakula ili kiendelee kuiva.

Pakua na ufurahie.

You can share this post!

UCHAMBUZI: Handisheki yakanganya viongozi wa ODM

Wakulima wa miche Nyeri waisihi serikali ya kaunti kuwa...

adminleo