• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 5:55 AM
Kiptanui anyakua ushindi Lisbon Half Marathon

Kiptanui anyakua ushindi Lisbon Half Marathon

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Erick Kiptanui ameibuka mshindi wa mbio za Lisbon Half Marathon jijini Lisbon, Ureno, Jumapili.

Kiptanui, ambaye alinyakua taji la mbio za kilomita 10 za San Silvestre Vallecana nchini Uhispania mnamo Desemba 31 mwaka 2017, ameshinda jijini Lisbon kwa saa 1:00:05.

Alifuatwa kwa karibu na raia kutoka Eritrea Yoahnes Gebregergish (1:00:16) naye Mkenya Morris Gachaga (1:00:17) akafunga mduara wa tatu-bora.

Bingwa mara tatu Zersenay Tadese (Eritrea), ambaye anashikilia rekodi ya dunia ya mbio za kilomita 21 ya dakika 58:23 aliyoweka jijini Lisbon mwaka 2010, pamoja na bingwa wa mwaka 2016 Sammy Kitwara (Kenya) ni baadhi ya wakiambiaji walijiandikisha kushiriki makala haya ya 28 waliomaliza nje ya tatu-bora.

Nafasi tatu za kwanza katika kitengo cha wanawake zimenyakuliwa na Waethiopia Etagegne Woldu (saa 1:11:27), Belainesh Oljira (1:11:29) na Helen Bekele (1:11:33).

You can share this post!

Klabu zilizopandishwa zakosa ustadi unaohitajika ligi ya...

Wakenya Maritim na Chebitok watawala Barcelona Marathon

adminleo