Michezo

Raga ya Wanawake: Kocha Felix Oloo akitaja kikosi kitakachokabiliana na Uganda

June 19th, 2019 Kusoma ni dakika: 2

Na GEOFFREY ANENE

KOCHA Mkuu wa timu ya raga ya wachezaji 15 kila upande ya wanawake, Felix Oloo ametaja kikosi kitakachovaana na wenzao kutoka Uganda katika kipute cha Elgon Cup Juni 22 uwanjani Mamboleo mjini Kisumu.

Kenya Lionesses ilishinda makala ya mwaka 2015 japo kwa jasho kwa jumla ya alama 12-11 baada ya kukabwa 5-5 na Lady Cranes jijini Nairobi na kutamba 7-6 jijini Kampala, na itakuwa mawindoni kutetea ubingwa.

Lionesses inajivunia kutwaa mataji ya Elgon Cup mwaka 2009, 2010, 2012, 2014 na 2015 nayo Uganda ilishinda mwaka 2006, 2008 na 2013.

Oloo alitaja kikosi cha wachezaji 23 watakaofanyia kazi Kenya katika mchuano huo muhimu Jumanne, Oloo alisema, “Tuna imani kubwa katika kikosi tulichochagua kuwakilisha Kenya. Uganda ina washambuliaji wazito na italenga kuonyesha ujuzi wake wa kulinda ngome yake. Hata hivyo, Lionesses iko imara kukabiliana nao.”

Aliongeza, “Lengo letu kubwa ni kuingia Kombe la Dunia baadaye mwaka huu katika mashindano ya kufuzu yatakayoandaliwa nchini Afrika Kusini. Wachezaji wamekuwa na bidii na wameonyesha wana hamu kubwa ya kuvalia jezi ya Kenya na kuwakilisha nchi vilivyo katika Elgon Cup na mashindano mengine.”

Lady Cranes inatarajiwa kuwasili mjini Kisumu mapema Alhamisi. Mechi kati ya Lionesses na Lady Cranes itaanza saa saba na nusu Jumamosi. Bei ya tiketi za mapema ni Sh400, huku zile za siku ya mashindano zikinunuliwa kwa Sh500. Tiketi za watu mashuhuri ni Sh1500.

Vikosi

Lionesses: 1. Juliet Nyambura (Northern Suburbs), 2. Staycy Atieno (Mwamba), 3. Imogen Hooper (Northern Suburbs) – (VC), 4. Enid Ouma (Homeboyz), 5. Bernedate Oleisia (Shamas), 6. Janet Awino (Homeboyz, nahodha msaidizi), 7. Mitchelle Akinyi (Impala Saracens), 8. Leah Wambui (Homeboyz), 9. Irene Otieno (Homeboyz), 10. Grace Adhiambo (Nakuru), 11. Jamari Agatha (Mwamba), 12. Philadelphia Orlando (Northern Suburbs, nahodha), 13. Celestine Masinde (Mwamba), 14. Christabel Lindo (Impala Saracens), 15. Janet Okelo (Mwamba), 16. Knight Otuoma (Kisumu), 17. Everlyne Kalimera (Mwamba), 18. Mercy Migongo (Homeboyz), 19. Emma Awuor (Homeboyz), 20. Anjeline Apiyo (Nakuru), 21. Veronicah Wanjiku (Nakuru), 22. Sophie Ayieta (Homeboyz), 23. Stella Wafula (Impala Saracens).

Uganda: 1. Faith Namugga, 2. Yvonne Najjuma, 3. Christine Nakayiza, 4. Charity Atimango, 5. Helen Gizamba, 6. Mary Gloria Ayot, 7. Winnie Atyang (nahodha), 8. Beatrice Atim Lamunu, 9. Samiya Ayikoru, 10. Charlotte Mudoola, 11. Christine Akello, 12. Peace Lekuru (nahodha msaidizi), 13. Aisha Nakityo Nabulime, 14. Ritta Nadunga, 15. Mary Adoi Kyoita. Wachezaji wa akiba – 16.Peace Mirembe, 17. Warry Ssenfuka Joanita, 18. Fortunate Irankunda, 19. Irene Ziggy, 20. Lydia Namabiro, 21. Juliet Nandawula, 22. Diana Kwagala Anguchia, 23. Esther Tino.