Michezo

AFCON 2019: Fahamu vikosi vya timu zinazoshiriki

June 20th, 2019 Kusoma ni dakika: 9

Na GEOFFREY ANENE

MWANASOKA bora barani Afrika mwaka 2017 na 2018 Mohamed Salah (Misri) pamoja na mwenzake kutoka Liverpool Sadio Mane (Senegal) ni baadhi ya wachezaji wakali wanaotarajiwa kunogesha Kombe la Afrika (AFCON) litakalong’oa nanga nchini Misri mnamo Juni 21 kwa kudumu kwa siku 29.

Wachezaji wengine nyota wanaotarajiwa kutegemewa na timu zao katika makala haya ya 32 ni Victor Wanyama (Kenya), Riyad Mahrez (Algeria), Asamoah Gyan (Ghana), Mbwana Samatta (Tanzania), Eric Maxim Choupo-Moting (Cameroon), Moussa Marega (Mali), Taha Yassine Khenissi (Tunisia), Manfred Starke (Namibia), Percy Tau (Afrika Kusini), Wilfried Zaha (Ivory Coast), Hakim Ziyech (Morocco) na Ayub Timbe (Kenya).

Baadhi ya wachezaji ‘wazee’ katika makala haya ni makipa Nabii Yattara kutoka Guinea, 35, na nahodha wa Uganda Denis Onyango, 34, mshambuliaji Faneva Ima Andriatsima, 35, na beki Jeremy Morel, 35, (Madagascar), kiungo Mkenya Dennis Omino Odhiambo (34), viungo kutoka Morocco Mbark Boussoufa na Karim El Ahmadi (wote 34), kiungo wa Ivory Coast Serey Die (34), kiungo wa Afrika Kusini Hlompho Kekana (34) na raia wa Benin Stephane Sessegnon (35), Fabien Farnolle (34) na Mickael Pote (34).

Kipa wa Misri Essam El Hadary anashikilia rekodi ya mchezaji mzee kuwahi kushiriki AFCON.

Alidakia Mafirauni katika makala ya mwaka 2017 akiwa na umri wa miaka 44 na siku 21.

Wachezaji walio na umri mdogo katika mashindano haya ni Mkenya Ovella Ochieng (19), mshambuliaji Mohamed Amissi (18) na kipa Jonathan Nahimana (19) wote kutoka Burundi, Mualgeria Hicham Boudaoui (19), kipa Metacha Mnata na kiungo Yahya Zayd (wote 20) kutoka Tanzania, beki Mmoroko Achraf Hakimi (20), mshambuliaji Sekou Koita na kiungo Cheick Doucoure (wote 19 kutoka Mali) na kipa wa Guinea-Bissau Edimar Vieira Ca (18).

Mchezaji mwenye mdogo kuwahi kushiriki AFCON anasalia kuwa mshambuliaji Shiva N’Zigou kutoka Gabon aliyenogesha mashindano haya mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 16 na siku 93.

Hivi hapa vikosi vya mataifa 24 yatakayokusanyika nchini Misri kwa mashindano haya yanayofanyika kila baada ya miaka miwili.

VIKOSI VYA AFCON 2019

ALGERIA: Makipa – Azzedine Doukha (Al Raed), Rais M’Bolhi (El Etifaq), Alexandre Oukidja (Metz), Mabeki – Ramy Bensebaini, Mehdi Zeffane (Rennes), Youcef Atal (Nice), Djamel Benlamri (Al Shabab), Mohamed Fares (SPAL), Rafik Halliche (Moreirense), Aissa Mandi (Real Betis), Mehdi Tahrat (Lens); Viungo – Mehdi Abeid (Dijon), Ismail Bennacer (Empoli), Hicham Boudaoui (Paradou), Sofiane Feghouli (Galatasaray), Adlene Guedioura (Nottingham Forest); Washambuliaji – Youcef Belaili (Esperance), Yacine Brahimi (Porto), Baghdad Bounedjah (Al Sadd), Riyad Mahrez (Manchester City), Adam Ounas (Napoli), Islam Slimani (Fenerbahce).

ANGOLA: Makipa – Toni Cabaça (Agosto), Landu (Interclube), Ndulu (Desportivo da Huila); Mabeki – Isaac, Dani Massunguna, Paizo (Agosto), Edy Afonso (Petro de Luanda), Wilson (Petro de Luanda), Bastos (Lazio), Jonathan Buatu (Rio Ave), Bruno Gaspar (Sporting); Viungo – Herenilson (Petro de Luanda), Show, Macaia (Agosto), Stelvio Cruz (Dudelange), Djalma Campos, Freddy (Antalyaspor), Geraldo (Al Ahly); Washambuliaji – Mabululo (Agosto), Mateus Galiano (Boavista), Wilson Eduardo (Sporting de Braga), Gelson Dala (Rio Ave/Sporting), Evandro Brandao (Leixoes).

BENIN: Makipa – Fabien Farnolle (Yeni Malatyaspor), Saturnin Allagbe (Niort), Cherif Dine Kakpo (Buffalos); Mabeki – Junior Salomon (Plateau United), Olivier Verdon (Sochaux), Khaled Adenon (Amiens) Moise Adilehou (Levadiakos), David Kiki (Red Star), Emmanuel Imorou (Caen) , Rodrigue Fassinou (ASPAC), Seidou Baraze (Yzeure); Viungo – Rodrigue Kossi (Club Africain), Jordan Adeoti (Auxerre), Mama Seibou (SC Toulon), Anaane Tidjani (US Ben Guerdane), Sessi D’Almeida (Yeovil Town), Stephane Sessegnon (Genclerbiligi); Washambuliaji – Mickael Pote (Adana Demirspor), Steve Mounie (Huddersfield), Desire Segbe Azankpo (Senica), Jodel Dossou (Vaduz), Cebio Soukou (Hansa Rostock), David Djigla (Niort).

BURUNDI: Makipa – MacArthur Arakaza, Justin Ndikumana (Sofapaka), Jonathan Nahimana (Vital’O); Mabeki – Omar Moussa (Sofapaka), Christophe Nduwarugira (Uniao Madeira), Omar Ngando (Kigali), Abdoul Karim Nizigiymana (Vipers), Frederic Nsabiyumva (Chippa United), David Nshimirimana (Mukura Victory); Viungo – Gael Bigirimana (hana klabu ), Gael Duhayindavyi (Mukura Victory), Pierre Kwizera (Al-Orouba), Shassir Nahimana (Al-Mujazzal), Enock Nsabumukama (Zesco United), Hussein Shabani (Coffee); Washambuliaji – Cedric Amissi (Al-Taawoun), Mohamed Amissi (Breda), Saido Berahino (Stoke City), Elvis Kasomba (Melbourne Victory), Laudit Mavugo (Napsa Stars), Francis Mustafa (Gor Mahia), Selemani Yamini Ndikumana (Al-Adalh), Fiston Abdoul Razak (JS Kabylie).

CAMEROON: Makipa – Andre Onana (Ajax Amsterdam), Fabrice Ondoa (Oostende), Carlos Kameni (Fenerbahce); Mabeki – Collins Fai (Standard Liege), Michael Ngadeu-Ngadjui (Slavia Prague), Ambroise Oyongo Bitolo (Montpellier), Yaya Banana (Panionios), Gaetan Bong (Brighton), Jean Armel Kana-Biyik (Kayserispor), Dawa Tchakonte (Mariupol); Viungo – Andre-Frank Zambo Anguissa (Fulham), Georges Mandjeck (Maccabi Haifa), Pierre Kunde Malong (Mainz), Arnaud Djoum (Hearts), Wilfrid Kaptoum (Betis Sevilla); Washambuliaji – Stephane Bahoken (Angers), Eric-Maxim Choupo-Moting (PSG), Karl Toko Ekambi (Villareal), Jacques Zoua (Astra), Clinton Njie (Marseille), Christian Bassogog (Henan), Joel Tagueu (Maritimo), Olivier Boumal (Panionos).

DR CONGO: Makipa – Parfait Mandanda (Dinamo Bucarest), Anthony Mossi (Chiasso), Ley Matampi (Al Nassr); Mabeki – DJuma Shabani (Vita Club), Christian Luyindama (Galatasaray), Arthur Masuaku (West Ham), Wilfried Abro (Mka Ankaragucu), Glody Ngonda (Vita Club), Marcel Tisserand (Wolfsboug), Bobo Ungenda (Primiero di Agosto); Viungo – Chadrac Akolo (Stuttgart), Merveille Bokadi (Standard Liege), Chancel Mangulu (Porto), Paul Mpoku (Standard Liege), Trésor Mputu (TP Mazembe), Youssouf Mulumbu (Kilmarnock); Washambuliaji – Britt Assombalanga (Middlesbrough), Cedric Bakambu (Beijing Guoan), Yannick Bolasie (Anderlecht), Jonathan Mpangi (Antwerp), Jackson Muleka (TP Mazembe).

MISRI: Makipa – Ahmed El-Shennawy (Pyramids), Mohamed El-Shennawy (Al Ahly), Mahmoud Gennesh (Zamalek); Mabeki – Ahmed Elmohamady (Aston Villa), Baher El-Mohamady (Ismaily), Ahmed Hegazi (West Bromwich Albion), Mahmoud Alaa, Mahmoud Hamdy El-Wensh (Zamalek), Ahmed Ayman Mansour, Omar Gaber (Pyramids), Ayman Ashraf (Al Ahly); Viungo – Tarek Hamed (Zamalek), Mohamed Elneny (Arsenal), Ali Ghazal (Feirense), Nabil Emad Dunga, Abdallah El-Said (Pyramids), Walid Soliman (Al Ahly), Mohamed Salah (Liverpool), Mahmoud Hassan Trezeguet (Kasimpasa), Amr Warda (Atromitos); Washambuliaji – Ahmed Ali (Arab Contractors), Marwan Mohsen (Al Ahly), Ahmed Hassan Kouka (Olympiacos).

GHANA: Makipa – Richard Ofori (Maritzburg United), Lawrence Ati-Zigi (Sochaux, France), Felix Annan (Asante Kotoko, Ghana); Mabeki – Andy Yiadom (Reading), Abdul Baba Rahman (Reims), Lumor Agbenyenu (Goztepe), Kassim Nuhu, (Hoffenheim), John Boye (Metz), Jonathan Mensah (Columbus Crew), Joseph Aidoo (Genk), Joseph Attamah (Basaksehir); Viungo – Mubarak Wakaso (Deportivo Alaves), Thomas Partey (Atletico Madrid), Kwadwo Asamoah (Inter Milan), Afriyie Acquah (Empoli), Andre Ayew (Fenerbache), Christian Atsu (Newcastle United), Samuel Owusu (Cukaricki), Thomas Agyepong (Hibernian); Washambuliaji – Asamoah Gyan (Kayserispor), Jordan Ayew (Crystal Palace, England), Caleb Ekuban (Trabzonspor), Kwabena Owusu (Leganes).

GUINEA: Makipa – Naby Yattara (Excelsior), Ibrahima Kone (Pau), Aly Keita (Ostersunds); Mabeki – Fode Camara (Gazelec Ajaccio), Issiaga Sylla (Toulouse), Ernest Seka (Nancy), Simon Falette (Eintracht Frankfurt), Ousmane Sidibe (Beziers), Baissama Sankoh (Caen), Mikael Dyrestam (Xanthi), Julian Jeanvier (Brendford); Viungo – Amadou Diawara (Napoli), Ibrahima Cisse (Fulham), Boubacar Fofana (Gaz Metan), Naby Keita (Liverpool), Mady Camara (Olympiakos); Washambuliaji – François Kamano (Bordeaux), Mohamed Yattara (Auxerre), Ibrahima Traore (Borussia Monchengladbach), Jose Kante (Gimnastic Tarragona), Idrissa Sylla (Zulte Waregem), Fode Koita (Kasimpasa), Sory Kaba (Dijon).

GUINEA-BISSAU: Makipa – Jonas Mendes (Academico Viseu), Rui Dabo (Fabril), Edimar Vieira Ca (UDIB); Mabeki – Rudinilson Silva (Kaunas Zal), Marcelo Djalo (Fulham) Juary Soares (Mafra), Mamadu Cande (Santa Clara), Tomas Dabo (Riete), Nanu Gomes (Maritimo), Eliseu Nadjack Soares (Rio Ave); Viungo – Sori Mane (Cova da Piedade), Mamadu Tunkara Pele (Monaco), Zezinho Lopes (Senica), Jorge Bura Norgueira (Aves), Joao Jaquite (Tondela), Moreto Cassama (Reims); Washambuliaji – Jorginho Intima (CSKA Sofia), Piqueti Djassi (Al Shoulla), Toni Silva (Ittihad of Alexandria), Mama Balde (Aves), Romario Balde (Academica), Frederic Mendy (Vitoria Setubal), Joseph Mendes (Ajaccio).

IVORY COAST: Makipa – Sylvain Gbohouo (TP Mazembe), Ali Badra (Free State Stars), Tape Ira (FC San Pedro); Mabeki – Serge Aurier (Tottenham), Wilfried Kanon (ADO The Hague), Wonlo Coulibaly (ASEC Mimosas), Ismael Traore (Angers), Mamadou Bagayoko (Red Star), Cheikh Comara (Wydad Casablanca), Souleyman Bamba (Rennes); Viungo – Jean-Philippe Gbamin (Mainz), Geoffrey Serey Die (Neuchatel Xamax), Jean-Michael Seri (Fulham), Victorian Angban (Metz), Franck Kessie (Milan) , Ibrahim Sangare (Toulouse); Washambuliaji – Max-Alain Gradel (Toulouse), Nicolas Pépé (Lille), Wilfried Zaha (Crystal Palace), Jonathan Kodjia (Aston Villa), Roger Assalé (Young Boys Bern), Maxwel Cornet (Lyon), Wilfried Bony (Without a club).

KENYA: Makipa – Patrick Matasi (St George), Faruk Shikalo (Bandari), John Oyemba (Kariobangi Sharks); Mabeki – David Owino (Zesco United), Musa Mohammed (Nkana), Bernard Ochieng (Vihiga United), Joseph Okumu (Real Monarch), Joash Onyango, Philemon Otieno (Gor Mahia), Eric Ouma (Vasalund), Aboud Omar (Sepsi); Viungo – Victor Wanyama (Tottenham Hotspur), Ismail Gonzalez (Las Palmas), Dennis Odhiambo (Sofapaka), Eric Johanna (Bromma), Francis Kahata (Gor Mahia), Paul Were (AFC Leopards), Johanna Omolo (Cercle Brugge); Washambuliaji – Ovela Ochieng (Vasalund), Ayub Timbe (Beijing Renhe), Michael Olunga (Kashiwa Reysol), John Avire (Sofapaka), Masoud Juma (hana klabu).

MADAGASCAR: Makipa – Melvin Andrien (Martigues), Ibrahima Dabo (Gobelins), Jean Randrianasolo (CNaPS Sport); Mabeki – Mamy Randrianarisoa, Pascal Razakanantenaina (St Pierroise), Dimitry Caloin (Les Herbiers), Thomas Fontaine (Reims), Romain Metanire (Minnesota),Jerome Mombris (Grenoble), Jeremy Morel (Lyon), Toaviina Rambeloson(Arras); Viungo – Ibrahim Amada (Mouloudia Alger), Anicet Andrianantenaina (Ludogorets), Andriamiraldo Andrianarimanana (Kaizer Chiefs), Marco Ilaimaharitra (Charleroi), Lalaina Nomenjanahary (Paris FC), Jean Rakotoarisoa (Fosa Juniors), Rayan Raveloson (Troyes); Washambuliaji – Charles Andriamahitsinoro (Al Aldalh), Faneva Andriatsima (Clermont), William Gros (Vitre), Tsilavina Njiva (Samut Sakhon), Paulin Voavy (Misr El-Makkasa).

MALI: Makipa – Djigui Diarra (Stade Malien), Adama Keita (Djoliba), Ibrahima Mounkoro (TP Mazembe); Mabeki – Mamadou Fofana (Metz), Massadio Haidara (Lens), Youssouf Kone (Lille), Boubacar Kiki Kouyate (Troyes), Falaye Sacko (Vitoria Guimaraes), Hamari Traore (Rennes), Molla Wague (Nottingham Forest); Viungo – Lassana Coulibaly (Rangers), Cheick Doucoure (Lens), Amadou Haidara (RB Leipzig), Diadie Samassekou (Salzburg), Adama Traore (Cercle Bruges); Washambuliaji – Kalifa Coulibaly (Nantes), Abdoulaye Diaby (Sporting), Moussa Djenepo (Southampton), Moussa Doumbia (Reims), Sekou Koita (Wolfsberg), Moussa Marega (Porto), Adama Niane (Charleroi), Adama Traore (Orleans).

MAURITANIA: Makipa – Souleimane Brahim (Nouadhibou), Namori Diaw (Kedia), Babacar Diop (Police); Mabeki – Abdoul Ba (Auxerre), Bakary Ndiaye (Difaa Hassani El Jadida), Sally Sarr (Servette Geneva), Diadie Diarra (Sedan), Harouna Sy (Grenoble), El Mostapha Diaw (Nouakchott Kings), Aly Abeid (Alcorcon), Abdoul Kader Thiam (Orleans); Viungo – Mohamed Dellah Yali (Tadjenanet), Ibrehima Coulibaly (Grenoble), Dialo Guidileye (Elazigspor), Khassa Camara (Xanthi), Alassane Diop (Hajer), Abdoulaye Gaye (Nouadhibou), El Hacen El Id (Real Valladolid); Washambuliaji – Adama Ba (Giresunspor), Ismael Diakhite (Tataouine), Moulaye Ahmed Khalil (AS Gabes), Souleymane Anne (Aurillac Arpajon), Hemeya Tanjy (Nouadhibou).

MOROCCO: Makipa – Mounir El Kajoui (Malaga), Yassine Bounou (Girona), Ahmed Reda Tagnaouti (Wydad Casablanca); Mabeki – Marouane Da Costa (Ittihad Jeddah), Ghanem Saiss (Wolverhampton), Mehdi Benatia (Al-Duhail), Achraf Hakimi (Dortmund), Abdelhamid Yunis (Reims), Noussair Mazroaui (Ajax), Abdelkarim Baadi (Hassania d’Agadir); Viungo – Karim El Ahmadi (Al Ittihad), Youssef Ait Bennasser (Saint Etienne), Moubarak Boussoufa (Al-Shabab), Younes Belhanda (Galatasaray), Faycal Fajr (Caen), Mehdi Bourabia (Sassuolo), Nordin Amrabat (Al-Nasr), Hakim Ziyech (Ajax), Youssef El-Nesyri (Leganes), Nabil Dirar (Fenerbache); Washambuliaji – Khalid Boutaib (Zamalek), Soufiane Boufal (Celta Vigo), Osama Idrissi (AZ Alkmaar).

NAMBIA: Makipa – Lloyd Kazapua (Maccabi), Maximilian Mbaeva (Golden Arrows), Ratanda Mbazuvara (African Stars); Mabeki – Ananias Gebhardt (Baroka), Charles Hambira (Tura Magic), Riaan Hanamub (Jomo Cosmos), Denzil Hoaseb (Highlands Park), Ivan Kamberipa (African Stars), Ryan Nyambe (Blackburn Rovers); Viungo – Ronald Ketjijere, Marcel Papama (African Stars), Willy Stephanus, Petrus Shitembi (Lusaka Dynamos), Dynamo Fredericks (Black Africa), Larry Horaeb (Tura Magic), Deon Hotto (Bidvest Wits), Absalom Limbondi (United Africa Tigers), Joslyn Kamatuka (Cape Umoya); Washambuliaji – Isaskar Gurirab (Life Fighters), Litamunua Keimuine (Dire Dawa City), Peter Shalulile (Highlands Park), Benson Shilongo (Ismaily), Manfred Starke (Jena).

NIGERIA: Makipa – Francis Uzoho (Anorthosis Famagusta), Ikechukwu Ezenwa (Katsina United F.C), Daniel Akpeyi (Kaizer Chiefs); Mabeki – Olaoluwa Aina (Torino), Abdullahi Shehu (Bursaspor), Chidozie Awaziem (Rizespor), William Ekong (Udinese), Leon Balogun (Brighton & Hove Albion), Kenneth (Leganes), Jamilu Collins (Paderborn); Viungo – John Obi Mikel (Middlesbrough), Wilfred Ndidi (Leicester City), Oghenekaro Etebo (Stoke City), John Ogu (Hapoel Be’er Sheva); Washambuliaji – Ahmed Musa (Al-Nassr), Victor Osimhen (Charleroi), Moses Simon (Levante), Odion Ighalo (Shanghai Shenhua), Henry Onyekuru (Galatasaray), Alex Iwobi (Arsenal), Samuel Kalu (Bordeaux), Paul Onuachu (Midtjylland), Samuel Chukweze (Villarreal CF).

SENEGAL: Makipa – Abdoulaye Diallo (Rennes), Alfred Gomis (Spal) and Edouard Mendy (Reims); Mabeki – Kalidou Koulibaly (Napoli), Moussa Wague (Barcelona), Pape Abdou Cisse (Olympiacos), Salif Sane (Schalke), Youssouf Sabaly (Bordeaux), Lamine Gassama (Goztepe), Saliou Ciss (Valenciennes), Cheikhou Kouyate (Crystal Palace); Viungo – Alfred Ndiaye (Malaga), Idrissa Gana Gueye (Everton), Keprin Diatta (Club Brugge), Pape Alioune Ndiaye (Galatasaray) and Henri Saivet (Bursaspor); Washambuliaji – Ismaila Sarr (Rennes), Keita Balde (Inter Milan), Mbaye Niang (Rennes), Moussa Konate (Amiens), Mbaye Diagne (Galatasaray), Sada Thioub (Nimes), Sadio Mane (Liverpool).

AFRIKA KUSINI: Makipa – Bruce Bvuma (Kaizer Chiefs), Darren Keet (Bidvest Wits), Ronwen Williams (SuperSport); Mabeki – Sifiso Hlanti, Thulani Hlatshwayo, Buhle Mkhwanazi (Bidvest Wits), Daniel Cardoso, Ramahlwe Mphahlele (Kaizer Chiefs), Innocent Maela (Orlando Pirates), Thamsanqa Mkhize (Cape Town City); Viungo – Hlompho Kekana, Tiyani Mabunda, Themba Zwane (Mamelodi Sundowns), Dean Furman (SuperSport), Thembinkosi Lorch (Orlando Pirates), Kamohelo Mokotjo (Brentford), Thulani Serero (Vitesse Arnhem), Bongani Zungu (Amiens); Washambuliaji – Lebogang Maboe, Sibusiso Vilakazi (Mamelodi Sundowns), Lebo Mothiba (Strasbourg), Percy Tau (Royal Union St Gilloise), Lars Veldwijk (Sparta Rotterdam).

TANZANIA: Makipa – Aishi Manula (Simba), Metacha Mhata (Mbao) na Aron Kalambo (TZ Prisons); Mabeki – Hassan Ramadan (Nkana), Vincent Phillipo (Mbao), Gadiel Michael (Young Africans), Ally Mtoni (Lipuli), Mohammed Hussein (Simba), Kelvin Yondani (Young Africans), Erasto Nyoni (Simba), Agrey Moris (Azam); Viungo – Feisal Salum (Young Africans), Himid Mao (Petrojet), Mudathir Yahya (Azam), Frank Domayo (Azam), Farid Mussa (Tenerife), Yahya Zayd (Ismaily); Washambuliaji – Rashid Mandawa (Botswana Defence Force), Mbwana Samatta (Genk), Thomas Ulimwengu (JS Saoura), John Bocco (Simba), Abdillanie Mussa (Blackpool), Simon Msuva (Difaa El Jadid).

TUNISIA: Makipa – Farouk Ben Mustapha (Al Shabab), Mouez Hassen (Nice), Moez Ben Cherifia (Esperance); Mabeki – Dylan Bronn (Gent), Yassine Meriah (Olympiacos), Oussama Haddadi (Dijon), Nassim Hnid (Sfaxien), Rami Bedoui (Al Faiha), Karim Aouadhi (Etoile du Sahel), Mohamed Drager (Paderborn), Wajdi Kechrida (Etoile du Sahel); Viungo – Ellyes Skhiri (Montpellier), Ferjani Sassi (Zamalek), Ayman Ben Mohamed (Esperance), Marc Lamti (Bayern Leverkusen), Ghailene Chaalai (Esperance), Bassem Srarfi (Nice), Youssef Msakni (Eupen), Naim Sliti (Dijon), Anice Badri (Esperance); Washambuliaji – Wahbi Khazri (Saint-Etienne), Taha Khenissi (Esperance), Firas Chaouat (CS Sfaxien).

UGANDA: Makipa – Denis Onyango (Mamelodi Sundowns), Jamal Salim (Al Hilal), Robert Odongkara (Adama City); Mabeki – Nico Wakiro Wadada (Azam), Brian Ronald Ddungu Mukiibi (Ostersunds), Murushid Jjuuko (Simba), Bevis Mugabi (Yeovil Town), Isaac Muleme (Viktoria Zizkov), Hassan Wasswa Mawanda (hana klabu ), Joseph Ochaya (TP Mazembe), Timothy Denis Awanyi (KCCA), Godfrey Walusimbi (hana klabu); Viungo – Mike Azira (Montreal Impact), Allan Kateregga (Maritzburg), William Kizito Luwagga (Shakhter Karagandy), Khalid Aucho (Church Hill Brothers), Faruku Miya (HNK Gorica), Abdul Lumala (Syrianska), Tadeo Lwanga (Vipers); Washambuliaji – Patrick Henry Kaddu (KCCA), Derrick Nsibambi (Smouha), Allan Kyambadde (KCCA), Emmanuel Arnold Okwi (Simba).

ZIMBABWE: Makipa – George Chigova (Polokwane City), Elvis Chipezeze (Baroka), Edmore Sibanda (Witbank Spurs); Mabeki – Teenage Hadebe (Kaizer Chiefs), Divine Lunga (Golden Arrows), Ronald Pfumbidzai (Bloemfontein Celtic), Tendai Darikwa (Nottingham Forest), Jimmy Dzingai (Power Dynamos), Alec Mudimu (CEFN Druids); Viungo – Talent Chawapihwa (Amazulu), Danny Phiri (Golden Arrows), Marshall Munetsi (Orlando Pirates), Marvelous Nakamba (Club Brugge), Tafadzwa Kutinyu (Azam), Ovidy Karuru (Amazulu), Khama Billiat (Kaizer Chiefs), Kudakwashe Mahachi (Orlando Pirates), Thabani Kamusoko (Young Africans); Washambuliaji – Knowledge Musona (Anderlecht), Nyasha Mushekwi (Dalian Yifang), Tinotenda Kadewere (Le Havre), Knox Mutizwa (Golden Arrows), Evans Rusike (SuperSport United).