• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Tofauti za upataji wa lugha ya kwanza na lugha ya pili na maandalizi ya mbinu za ufundishaji

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Tofauti za upataji wa lugha ya kwanza na lugha ya pili na maandalizi ya mbinu za ufundishaji

Na MARY WANGARI

KUNA tofauti kubwa kati ya upataji wa lugha ya kwanza na lugha ya pili.

Kila mtu ana lugha ya kwanza. Wataalamu wanaounga mkono kauli hii ni pamoja na Ellis (1994) na Bley Vroman (1988).

Wataalamu hawa wanaainisha hoja tisa kama zifuatazo:

Mafanikio kwa ujumla – mtoto anapopata lugha ya kwanza huipata lugha ile kwa usahihi katika nyanja zote. Japo anaweza asiweze kutofautisha uchambuzi kiisimu lakini wapataji lugha ya pili hupata mafaniko katika maeneo fulani fulani tu katika lugha wanayojifunza..

Kushindwa (failure) – katika upataji wa lugha ya kwanza kushindwa hakupo labda ikiwa ana ulemavu fulani lakini kwa wapataji lugha ya pili kushindwa ni jambo la kawaida.

Utofauti baina ya wanajifunza /wapataji lugha (variation) – wanaopata lugha ya kwanza hawana tofauti yoyote katika upataji lugha, kumaanisha kwamba wakifikia umri fulani labda kama miaka mitatu hivi wote watakuwa wamepata.

Endapo atakuwa hajapata lugha hadi umri wa miaka tisa basi huyo atakuwa na matatizo (msukuku-kukoma kujifunza lugha (fossilization)).

Hata hivyo, kuna tofauti kubwa mno miongoni mwa wanaojifunza lugha ya pili.

Hii ni kwa sababu unaweza ukapata kozi inapokamilka kuna ambaye amemudu na mwingine bado.

Malengo/goals – lengo la mjipatiaji lugha ya kwanza ni umilisi wa lugha hiyo katika viwango vyote lakini lengo la mjipatiaji lugha ya pili ni kupata maudhui na umilisi kidogo.

 

MAANDALIZI YA MBINU ZA UFUNDISHAJI

Tofauti nyingine katika ujifunzaji lugha zinatokana na mambo kama:

Usukuku(ukakamaaji) – suala la usukuku halipo kwa mtoto anayejipatia lugha ya kwanza lakini kwa anayejipatia lugha ya pili hii ni hali ya kawaida kabisa. Anasema Han 1998-2013.

Uvumbuzi/ughamuzi – wajipatiaji wa lugha ya kwanza huendelea kujipatia lugha ya kwanza katika ughamzi bwete (kujisahihisha dosari pasipo kujua) lakini mpataji lugha ya pili huwa katika ughamzi tambuzi.

Maelekezo/instruction – ujipatiaji wa lugha ya kwanza hauhitaji maelekezo, labda kidogo kwa ajili ya kuchochea lakini mjipatiaji wa lugha ya pili anahitaji maelekezo ya kina na sahihi na kwa utaratibu maalumu.

Uthibitisho hasi – katika ujipatiaji wa lugha ya kwanza usahihishaji wa dosari haumsaidii mpataji wa lugha ya kwanza kupata lugha ile lakini katika upataji wa lugha ya pili ni muhimu kufanya masahihisho ili kumpa mwelekeo sahihi.

Athari hisivu (affective factor) – mjipatiaji wa lugha ya kwanza hakuna kitu kinachomwathiri kujipatia lugha ya kwanza kwa mfano hafikilii kwamba atakosea, atachekwa bali yeye hutamka tu lakini katika ujipatiaji wa lugha ya pili athari hisivu zina msaada sana katika kupata lugha. Kwa mfano, mwanafunzi mcheshi, huenda atapata lugha haraka kuliko mnyamavu.

Muda – Mtoto huchukua muda mfupi kati ya miezi 36 na anakuwa mmilisi wa lugha lakini mjipatiaji wa lugha ya pili hutumia muda mrefu sana ambapo inaweza ikafika miaka tisa.

 

KUANDAA SOMO:

Hapa tunaangalia muundo wa andalio la somo (lesson plan) unahitaji kuangalia mambo haya:

  1. Muda
  2. Mada
  3. Malengo- kitu gani kitokee katika somo hilo. Kwa mfano mwisho wa somo mwanafunzi aweze kutaja aina ya ‘nomino’
  4. Mazingira/muktadha- darasa, aina ya wanafunzi.
  5. Shajara
  6. Logbook

You can share this post!

Nigeria kuingia uwanjani dhidi ya limbukeni Burundi mechi...

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Muundo wa andalio la somo

adminleo