• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 5:55 AM
Migne alia Harambee Stars ilikosa mastaa wazoefu

Migne alia Harambee Stars ilikosa mastaa wazoefu

Na JOHN ASHIHUNDU

Baada ya kuchapwa 2-0 na Algeria, kocha Sebastien Migne amesema timu yake ya Harambee Stars ilikosa wachezaji wazoefu katika mechi hiyo.

Stars walifungwa bao la kwanza dakika ya 34 kutokana na mkwaju wa penlti kupitia kwa Baghdad Bounedjah baada ya Dennis Odhiambo kumchezea ngware Youcef Atal katika eneo la hatari.

Bao la pili lilipatikana kupitia kwa Riyadh Mahrez wa klabu ya Manchester City ambaye kombora lake lilimchanganya beki wa kushoto Aboud Omar kabla ya kuingia.

“Kwa hakika tilikosa wachezaji wa uzoefu wa kukabiliana na Algeria. Baadhi yao waliogopa kwa vile hiyo ilikuwa mara yao ya kwanza kucheza mechi kubwa,” alisema Migne

“Baada ya kufungwa bao la pili nilishuhudia baadhi yao wakipoteza matumaini. Hata hivyo, tumejifunza mengi kutokana na mechi hiyo ya kwanza. Tuliwapa wapinzani wetu nafasi kubwa ya kutawala uwanjani.”

Stars watarejea uwanjani dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania Alhamisi kwa mechi ya pili kabla ya kuvaana na Senegal katika mechi ya mwisho kudini.

You can share this post!

Sasa nataka ubingwa wa EPL, Klopp asema

Eto’o amshauri Salah ajiunge na Barca

adminleo