• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
SIHA NA LISHE: Manufaa ya kula parachichi

SIHA NA LISHE: Manufaa ya kula parachichi

Na MARGARET MAINA

[email protected]

PARACHICHI ni tunda ambalo lina mafuta mengi na yenye manufaa makubwa kiafya.

Tunda hili limesheheni manufaa makubwa katika afya ya mwanadamu.

Parachichi limejaa virutubisho mbalimbali

Kalori, madini ya sodium, wanga, Vitamini K, Vitamini C, madini ya Potasiamu Vitamini B5, Vitamini B6, Asidi ya Folate, Vitamini E nio baadhi tu ya vinavyopatikana katika tunda hili.

Virutubisho vyote hivi ni muhimu kwa ajili ya mwili kujijenga na kujilinda dhidi ya magonjwa.

Lina virutubisho vitokanavyo na mimea

Carotenoids inayopatikana kutoka kwenye parachichi ina manufaa makubwa kwa ajili ya miili yetu katika kulinda macho dhidi ya matatizo mbalimbali yakiwemo yale yatokanayo na umri kusonga.

Lima Persenones A na B inayozuia uvimbe mwilini.

Juisi ya parachichi. Picha/ Margaret Maina

Parachichi lina Fatty Acid

Fatty Acid ni asidi itokanayo na mafuta ya parachichi ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya shughuli mbalimbali katika miili yetu. Asidi hii inahitajika katika uzalishaji wa homoni na ukuaji wa seli.

Hupunguza lehemu mbaya (cholesterol)

Mafuta ya lehemu ni hatari ikiwa kiwango chake kitakuwa kingi mwilini. Mafuta haya husababisha matatizo mbalimbali hasa maradhi ya moyo.

Matunda ya parachichi hayana lehemu mbaya inayoweza kuathiri afya yako.

Kukabili maradhi ya kisukari

Parachichi ni tunda ambalo kiwango chake cha sukari hakina athari hasi kwenye mwili. Hivyo basi utumiaji wa parachichi utakuwezesha kuweka kiwango cha sukari mwilini kuwa katika hali nzuri ya wastani.

Hulinda afya ya macho

Kemikali ya lutein na zeaxanthin ni muhimu sana kwa ajili ya kulinda na kuimarisha afya ya macho.

Ikumbukwe kuwa parachichi ni tunda lenye kiasi kikubwa cha lutein ambayo pia hulinda macho dhidi ya matatizo mbalimbali yatokanayo na umri.

Parachichi lina Potasiamu nyingi

Potasiamu ni muhimu katika miili yetu kwani hutuwezesha kutawala kiwango cha sodiamu katika miili yetu na kutuepusha na madhara yatokanayo na madini haya ya sodiamu.

Huboresha afya ya nywele na ngozi

Naamini umewahi kusikia kuwa parachichi hutumika kutengenezea mafuta ya nywele na ya ngozi; hii ni kutokana na kusheheni vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya ya nywele na ngozi zetu.

Hivyo badala kununua mafuta ya gharama kubwa ili kupata vitamini E kwa ajili ya ngozi na nywele zako, kula tunda la parachichi.

Huimarisha mifupa

Kutokana na parachichi kuwa na vitamini K pamoja na madini ya kopa na folate ambavyo ni muhimu kwa ajili ya mifupa, tunda hili linakuwa na nafasi kubwa katika kuimarisha mifupa.

Huboresha mmeng’enyo wa chakula

Vyakula vyenye nyuzinyuzi ni muhimu sana kwa ajili ya kuufanya mmeng’enyo wa chakula uende vizuri. Parachichi ni tunda lenye nyuzinyuzi

Huimarisha kinga ya mwili

Kinga ya mwili hutegemea vitamini B, C na E ili kujiimarisha na kujijenga. Hivyo ulaji wa parachichi utaimarisha kinga ya mwili yako kwani parachichi limesheheni vitamini B, C na E.

Huboresha afya ya ubongo

Madini ya kopa yanayopatikana kwenye parachichi yana nafasi kubwa sana katika kuufanya ubongo ufanye kazi vyema.

Huongeza nguvu za mwili

Miili yetu inategemea sana wanga, protini na mafuta ili kupata nguvu. Tunda la parachichi ni chanzo kikubwa cha virutubisho hivi vitatu.

Hivyo kuongeza parachichi katika mlo wako kutakuwezesha kuuongezea mwili wako nguzu zaidi.

You can share this post!

Kwaheri Bob

SOKA MASHINANI: Kiranga United FC

adminleo