Makala

MAPISHI: Chipsi na kuku

July 3rd, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa kupika: Nusu saa

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • Kuku kilo 1
  • Viazi ulaya kilo 1
  • Nyanya 2 zilizoiva vizuri
  • Kitunguu saumu ¼ kijiko
  • Tangawizi ¼ kijiko
  • Majani ya giligilani
  • Chumvi ½ kijiko
  • Pilipili manga kijiko 1
  • Mafuta ya kupikia
  • Apple cider vinegar ½ kikombe
  • Kitunguu maji 1

Maelekezo

Menya viazi kisha kata ukubwa wa chipsi unaopenda.

Viazi ambavyo havijamenywa. Picha/ Margaret Maina

Viweke kwenye maji yaliyotiwa chumvi.

Safisha kuku vizuri kisha weka kwenye sufuria safi. Mwagia vinegar juu yake.

Bandika sufuria ya kuku mekoni. Acha ichemke vizuri. Kisha toa na uhifadhi.

Bandika kikaangio motoni, weka mafuta ya kupikia.

Mafuta yakishapata moto, weka viazi na kaanga hadi chipsi ziive.

Epua na urudie hadi viazi vyote viwe vimepikwa.

Chipsi tayari kuliwa. Picha/ Margaret Maina

Kaanga kuku kwenye mafuta uliyotumia kupikia chipsi.

Bandika sufuria mekoni, mimina mafuta. Yakipata moto, weka kitunguu maji na viungo vyote ila usiweke nyanya.

Vitunguu vikianza kubadilika rangi, weka nyanya. Nyanya zikiwa tayari, weka kuku na funika vizuri kwa dakika tano.

Ongeza supu ya kuku nusu kikombe kwenye sufuria; acha ichemke.

Weka chipsi kwenye sufuria yenye sosi ya kuku. Pika hadi supu ikaukie.

Epua, pakua na ufurahie.