MAPISHI: Vitumbua
Na MARGARET MAINA
VITUMBUA ni aina ya mikate midogo ya mviringo iliotengenezwa kwa unga wa mchele na sukari na kukaangwa.
Muda wa kuandaa: Dakika 10
Muda wa kupika: Dakika 20
Walaji: 5
Vinavyohitajika
- unga wa ngano nusu kilo
- tui la nazi vikombe viwili
- mayai 3
- sukari ½ kikombe
- iliki kijiko 1
- mafuta ya kupikia
- hamira nusu kijiko
- vikombe 2 vya mchele
Maelekezo
Osha na uloweke mchele usiku kucha. Chuja maji, weka pembeni.
Chemsha tui la nazi mpaka maji yake yawe ya ufufutende katika moto wa wastani.
Katika blenda, weka mchele, tui la nazi, iliki, sukari, chumvi na hamira. Saga mpaka upate mchanganyiko uliolainike vizuri kisha mimina mchanganyiko kwenye bakuli.
Funika bakuli, acha mchanganyiko uumuke kwa muda wa saa moja.
Weka kikaangio chenye mafuta ya kupikia katika meko yenye moto wa wastani.
Mwagia mchanganyiko kiasi kiasi kwenye kikaangio cha vitumbua katika moto huo wa wastani.
Weka mafuta kwenye kila shimo la chuma cha vitumbua.
Mwagia mchanganyiko ujazo wa robo tatu ya kila shimo.
Acha vitumbua vianze kuiva kwa dakika tatu au mpaka vianze kuwa na rangi ya kahawia na kona zianze kukauka kiasi.
Kwa kutumia kijiti kama cha mishikaki, geuza kitumbua upande wa pili.
Acha vitumbua viive kwa dakika zingine tatu au mpaka viwe na rangi ya kahawia.
Epua vitumbua, weka kwenye bakuli lenye tissues au serviettes za jikoni ili mafuta yachujike.
Waweza pia kutumia nyaya za gauze kwa lengo ya kuhakikisha vitumbua vinakauka bila kuchukua vipande vya karatasi hizi ambazo zinaweza kuwa hatari kwa afya ya mlaji.
Pakua na ufurahie.