Habari

Waiguru mke halali wa wakili Waiganjo

July 13th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MWANGI MUIRURI

UWANJA wa shule ya msingi ya Kiamugumo ulifurika watu kutoka kila kona ya nchi kushuhudia Gavana Anne Mumbi Waiguru akifunga pingu za maisha na mpenzi wake, Wakili Kamotho Waiganjo.

Wanasiasa, viongozi wa kidini, wapigakura wa kawaida na Wazee wa Baraza la Agikuyu walitangamana Jumamosi wakiwa chonjo kuwa mashahidi  wa wawili hao wakifunga ndoa kitamaduni.

Waiguru na Waiganjo wakiwa mbioni kutinga umri wa miaka 60 ya uhai wao waliamua kufanya harusi yao kwa kuzingatia mila na desturi za jamii ya Agikuyu kuhusu ndoa.

Naibu Gavana wa Kirinyaga, Peter Ndambiri awali alikuwa ameambia Taifa Leo kuwa hafla hiyo ingehudhuriwa na watu 25,000.

Wageni

Rais Uhuru Kenyatta, kiongozi wa ODM, Raila Odinga, makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka ni miongoni mwa wageni waliohudhuria.

Waiganjo na Waiguru wanaingia kwa mkataba wa ndoa kwa mara moja tena zaidi kila mmoja baada ya kutalakiana na wa awali na ambapo wamejaliwa watoto ambao kwa sasa ni wakubwa.

Kumekuwa na mlo, vinywaji na densi kwa wingi.

Rais Uhuru Kenyatta, kiongozi wa ODM, Raila Odinga, makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka ni miongoni mwa wageni waliohudhuria harusi ya kitamaduni ya Gavana Anne Waiguru na Wakili Kamotho Waiganjo. Picha/ PSCU

Muhimu zaidi pia ni kwamba wengi wamejipamba mavazi ya kitamaduni.