• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 8:27 PM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Mchakato wa mawasiliano, nyenzo na aina za mawasiliano

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Mchakato wa mawasiliano, nyenzo na aina za mawasiliano

Na MARY WANGARI

MTUMA-UJUMBE au ukipenda mzungumzaji ana habari ambayo angependa kuiwasilisha na anaufuma ujumbe katika ishara kisha mtuma-ujumbe huupitisha au huutuma ujumbe kupitia njia fulani kama vile maongezi au maandishi.

Baadaye mpokeaji huufumua ujumbe kama vile kuusoma au kusikiliza kwa makini na kujaribu kufasiri maana ya mtuma-ujumbe. Kwa upande wake Davis (1976:22), anaelezea mawasiliano kama upitishaji wa habari na maelewano kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine.

Aidha, anafafanua kwamba mawasiliano ni mfumo wa kijamii. Kwa kuzingatia mawazo ya wataalam hawa ni dhahiri kuwa mawasiliano ni usafirishaji wa ujumbe kwa mtuma-ujumbe hadi kwa mpokea –ujumbe kwa kutumia nyenzo fulani.

Kwa mujibu wa Sperber & Willson (1995), wanasema kuwa mawasiliano kwa muktadha, unaweza kuchukuliwa kama sehemu tu yayanayodhaniwa kuhusu dunia na anayepokea habari.

Nyenzo za mawasiliano

Nyenzo mbalimbali zinazotumika kuwasilisha ujumbe zinajumuisha:

i. picha

ii. michoro

iii. lugha

iv. ngoma

v. miondoko ya mwili

Aina za Mawasiliano

Mawsiliano ya binadamu yanaweza kuorodheshwa katika vitengo viwili:

i. Mawasiliano finyu

ii. Mawasiliano timilifu.

Mawasiliano finyu

Mawasiliano haya yanahusisha usafirishaji wa habari au ujumbe kama vile mawazo, maarifa, ujuzi na kadhalika miongoni mwa watu kwa njia ya kauli, taarifa, redio, televisheni, magazeti na kadhalika.

Katika kitengo hiki cha mawasiliano, uwasilishaji ni wa mkondo mmoja unaoelekea upande mmoja.

Mtoa habari ana dhima ya kutoa habari tu na hapokei majibu au habari yoyote kutoka kwa mpokeaji.

Naye mpokeaji kwa upande wake anapokea tu bila kutoa habari yoyote. Hivyo basi aina hii ya mawasiliano ni rahisi na ya haraka kwa mtuma-ujumbe.

Mawasiliano yanaweza kufanywa kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na maongezi, maandishi, picha au mchoro pamoja na njia ya electroniki.

Kwa mfano, mawasiliano kwenye magazeti huwa ni ya kutimiza haja.Wananafsia hudai kuwa kimaumbile sisi ni wanyama wa kijamii. Hii ina maana kwamba tunawahitaji watu wengine sambamba na vile tunavyohitaji chakula.

Iwapo watu watatengwa bila kuwasiliana, watapata matatizo kwani watazongwa na mawazo na hata kukosa uwezo wa kuingiliana kijamii.

 

[email protected]

Marejeo

Adegbija, E. (1999). “Titbits on Discourse Analysis and Pragmatics” in the English and Literature in English. An Introduction. Unilovin: Department of Modern European Languages, Unilovin.

Anderson, J. A & Meyer, T.P. (1988). Mediated Communication: A social interaction perspective. Newsbury Park, CA: Sage.

Askew, K. (2003). Performing the Nation: Swahili Music and Cultural Politics. Dar es Salaam: Kapsel.

You can share this post!

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Vibainishi vya kimsingi katika...

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Dhana ya tamathali za usemi...

adminleo